Sunday, May 5, 2013

0

AMANI INAENDA WAPI WATANZANIA??? | TAARIFA KUHUSU MLIPUKO WA BOMU KANISANI OLASITI, ARUSHA

Posted in
UPDATES::::

Mbunge Lema amefika eneo la tukio, na baada ya yeye kufika wananchi wanaonekana kutabasamu.
Mbunge anasema: Poleni kwa yaliowakuta, Hakuna mwizi anaweza kurusha bomu ila uchunguzi ufanywe, na anasema anadhani polisi watamkamata haraka kama walivyomkamata yeye.

RPC asema, Mtu alitokea eneo la nyuma la kanisa akiwa amevalia kanzu na kulirusha bomu hilo..
-Na mejeruhi wapo zaidi ya 30, huku wakiwa na majeraha tofauti na wamepelekwa hospitali.
-Kuna majina yametajwa, ila hawayaweki hadharani kwa sababu za kiusalama.

MKUU WA MKOA ARUSHA ATOA POLE ZAKE huku akisema wameitwa wataalam mbalimbali ambao watafanya uchunguzi huo, huku pia akiomba utulivu na amani iwepo kipindi hichi cha upelelezi.
------------------------------------------------------------------------------

Kanisa katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti Arusha ambalo leo hii lilikuwa linapandishwa hadhi na kuwa Parokia limelipuliwa na  kitu  kinachosemekana  kuwa  ni  bomu, watu wengi wamejeruhiwa  na  mtu  mmoja  inasemekana  amefariki  dunia.

Tukio  hilo  limetokea  wakati  Misa ikiwa ndio inaanza .Ilikuwa ni saa 5 kamili...Kabla Askofu hajaanzisha sala , mlipuko mkubwa  ulitokea  ndani  ya  kanisa  hilo. 

Kanisa hilo lilikua likizinduliwa na Askofu Josephat Lobulu akiwa na balozi wa Vatican Francisco Padilla , Tanzania.

Kuna taarifa ambazo zinasema alionekana mtu akilirusha na kisha kukimbia ambapo alisema kijana mdogo aliyekuepo eneo hilo, na baadae tena ukaskika mlipuko mwingine ambao haukua wa nguvu kama ule wa mwanzo.

CHANZO CHA BOMU HILO INASEMEKANA KUWA KUNA  GARI AINA YA HIACE ILIFIKA KANISANI HAPO NA KUSIMAMA BAADAE AKASHUKA MTU ALIYEKUWA AMEVALIA VAZI MITHILI YA KANZU NA KURUSHA BOMU HILO, BALOZI WA PAPA NCHINI NDIYE ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA NA AMENUSURIKA KATIKA BOMU HILO ILA WATU WENGI WAMEJERUHIWA ZAIDI . 

ENDELEA KUWA NASI HAPAHAPA KWA TAARIFA ZAIDI

Mda si mrefu Askofu na mgeni wake wamesindikizwa kwa usalama mkubwa kutoka eneo la tukio.

AMANI inazidi toweka siku zinavyozidi kwenda, Watanzania tunaeleka wapi??? Mhm, Nadhani watu wa usalama watafanya uchunguzi vyema.

#Na Straton Mo Panish : Maoni Juu Ya Mlipuko Parokiani Arusha

LENGO LAO NI MOJA TU,KUHAKIKISHA WANAIGAWANYA TANZANIA KIDINI..MIMI NAAMINI HAKUNA UPANDE HATA MMOJA KATI YA WAISLAMU AMA WAKRISTO UNAOHUSIKA NA MATUKIO KAMA HAYA YA KISHETWANI..NI WATU FLANI TU WALIOPANDIKIZWA KUICHAFUA AMANI YA TZ KWA KIVULI CHA DINI,NA TUSIPOKUA MAKINI WANAELEKEA KUFANIKIWA KATIKA HILI..TUMEKUA WEPESI SANA KUAMINI MANENO MANENO YANAYOZUSHWA NA TUMEKUA WAGUMU MNO KUTUMIA AKILI NA UTASHI TULIOPEWA NA MWENYEZI MUNGU KUCHAMBUA NA KUTAMBUA MAMBO...

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ