Friday, August 16, 2013

0

BLANDINA CHAGULA A.K.A JOHARI KURUDI KIVINGINE: HUU NDO UTAKUA UJIO WAKE MPYA

Posted in ,
Ikiwa imepita miezi kama sio miaka kadhaa tangu mwanadada Blandina Chagula a.k.a Johari apotee machoni mwa watazamaji wa muvi za kibongo, ameamua kurudi tena kwenye uigizaji wa muvi hizo kivingine.



“Ijapokuwa watu walikuwa hawanioni lakini kazi za RJ company zilikuwa zinaendelea kutoka na zote nimeshiriki kikamilifu utengenezwaji wake na kwa namna nyingine ni kupisha tu vipaji vipya vipate kuonekana na sio kila siku ni Johari tu.” Johari aliliambia BK.

Kwa sasa Johari anashinda location kila siku na hadi sasa tayari amekamilisha muvi mbili ndani ya RJ ziitwazo Bad Luck ambayo amecheza bila Ray kuhusika kwa mara ya kwanza na nyingine ni Long Huck aliyocheza na Ray huku nyingine zikiwa zinamkosesha usingizi location kila siku.

“Labda niseme kwamba kwa mara ya kwanza, nimeshiriki filamu nje ya RJ na watu wengine kabisa kwa kunialika kwenye muvi zao huku nikishirikiana na chipukizi wengi.” Aliongeza Johari

Filamu alizoshirikishwa ni pamoja na Mke mchafu, Masumbuko nk. kitu ambacho hapo kabla hakuwahi kukifanya. Welcome again lady…!!!

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ