Jun
2013
20
WATUMIAJI WA SAMSUNG KUPATIWA ALBUM MPYA YA JAY-Z BURE
Posted in Jay-Z, Samsung, Samsung GalaxyRapper anaye set standard za Hiphop duniani Jay Z ametangaza ujio wa cd yake mpya Itakayoitwa Magna Carta Holy Grail, Itakuwa mtaani July 4 na kupitia Simu za Sumsung utaipata kirahisi zaidi. Watumiaji Milioni moja wa kwanza wa Samsung Galaxy III, Galaxy S 4, na Galaxy Note II watapata nafasi ya kuwa na application itakayo ruhusu kudownload cd hio. Application hii itakuwa tayari June 24 kupitia magnacartaholygrail.com .
Jay z amepokea Dolaa za Kimarekani Milioni 5 ili kugawa album hii kwa njia ya downloads kwa watumiaji milioni moja wa Samsung Galaxy III, Galaxy S 4, na Galaxy Note II. Njia nzuri ya kufanya biashara kwa msanii na kampuni ya simu.
Wakati wa game 5 ya NBA Finals walirusha clip inayo muonyesha Jay z akiwa na Rick Rubin, Pharrel Williams,Swizz Beats Na Timbaland wakitengeneza mzigo mwingine. Album ya Mwisho wa Jigga Ilikuwa The BluePrint 3 ya 2009
0 Maoni/comments: