Jun
2013
23
ONA JINSI MWANA-FA ALIVYOLAZIMISHWA KUTAJA JINA LA "JAY DEE" KATIKA SHOO
Posted in Lady Jay Dee, Mwana FA
Tofauti na ilivyozooeleka katika wimbo wa Mabinti, kwa mara ya kwanza Mwana FA aliruka jina la mwanamuziki Lady Jay Dee ‘Anaconda’, hali iliyowafanya mashabiki wamtake arudie tena na kutenda haki.
Mwana FA alisita kwa muda na baadaye aliamua kurudia wimbo huo na alipofika katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na tena.
" Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA. "
Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Awali shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu waliokuwa wamefika walikuwa kama 250 tu.
0 Maoni/comments: