JAY-Z KUUZA HISA ZAKE KATIKA YA NETS, NA KUANZA KUA WAKALA WA WACHEZAJI
Posted in Brooklyn Nets, Jay-Z
Mwanamuziki
nguli na tajiri yupo katika hatua za mwisho za kuuza hisa zake kwenye
timu ya mpira wa kikapu ya Brooklyn Nets ili aweze kuwa wakala wa
wachezaji wa NBA, ikiwezekana kabla ya mwisho wa msimu. Mpango huo kwa
sasa upo katika kuufanikisha, mtu mmoja mwenye ukaribu wa kambi ya Jay Z
alisema jana Jumatano.
Sheria za NBA zinakataza mtu yoyote mwenye miliki kwenye timu kufanya kazi ya uwakala kwa wachezaji.
Hivi
karibuni Jay Z kupitia kampuni take ya Roc Nation aliingia mkataba wa
ushirikiano na Creative Artists Agency (CAA) na matumaini yao ni kuanza
kushindani dili za kuwakilisha wachezaji wa NBA kuanzia mwezi June mwaka
huu.
Jay-Z
anamiliki asilimia chache sans kwenye timu ya Nets, lakini amesaidia
sans katika kuitangaza timu hiyo na kuihamisha kutoka New Jersey kwenda
Brooklyn. Alikuwa mstari wa mbele katika kukamilisha makao makuu ya timu
hiyo yenye thamani ya $1 billion ya Barclays Center, pia akisaidia
katika ubunifu wa jezi mpya za timu hiyo. Kisha akaizindua Barclays
Center kwa shows nane mfululizo kwa mafanikio kwa kuuza tiketi zote.
Jay
Z ambaye ni mume wa mwanamuziki Beyonce ana urafiki na wachezaji wengi
wakubwa wa NBA, Lebron James na winging kibao, kwa haraka Jay Z anaweza
kufanikiwa sans kwenye biashara hiyo ya uwakala.
Jay Z na kampuni yake mpya ya uwakala hivi karibuni alimsaini star wa New York Yankees All-Star Robinson Cano.
0 Maoni/comments: