Thursday, March 21, 2013

0

ALICHOKIANDIKA DOGO JANJA KUHUSU ELIMU YAKE

Posted in , ,

Mimi Abdul-Aziz Abubakari Chende ninae julikana kwasasa kama Janjaro ninaandika ujumbe huu uwaaendee waTanzania wote Mimi ni kijana Mwenye Umri Wa Zaidi ya Miaka 18 Ninasoma Shule Ya Makongo Kidato Cha tatu Baada ya Kuwa nimefaulu Kidato Cha pili Pia Vile Vile ninajihusisha na Kazi ya MZIKI" nikiwa katika Lebo ya MTANASHATI ENTERTIANMENT Chini ya OSTAZ JUMA NAMUSOMA....ninayatoa YA MOYONI Kazi yangu ya Mziki Ndio iliyofanya kila Mtanzania kunitambua kama mimi JANJARO nanikajizolea Mashabiki Wengi hivyo na kila Mtanzania kunitambua kama ABDUL-AZIZ au JANJARO nina Talent (KIPAJI) lakini sasa kipaji Icho kilitokea nikiwa na umri Mdogo ikiwa ninaSoma hivyo nlitokea kukipenda sana kipaji changu na kukithamini sana kwani ndicho kilichofanya kila mtanzania kunitambua na pia mziki huo huo uliweza kusababisha mimi kuonana na viongozi Wakubwa Wakubwa katika Serikali Mojawapo Akiwa MH RAIS WETU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA...JAKAYA MRISHO KIKWETE amenitambua mimi kama JANJARO sababu ya MZIKI kwahiyo nitauheshimu mziki na kuupenda na kuendelea kuthamini kwa sababu umenifikisha mbali MACHUNGU yananiingia MOYONI nakunifanya KUWA MNYONGE kwa Baadhi ya WATANZANIA Ambao hawapendi Maendeleo yangu na Mafanikio yangu kutumia Shule ni Kigezo cha Kuniponda,kuniDhalilisha,kunitukana,na baadhi ya Watu wengine Wenye mitandao kama WebSite au Blog na Facebook,Kuandika habari Zisizo kuwa na Uchunguzi na Uhakika Kwakua ni wavivu wa kutafuta habari wakikurupuka tu kitandani wanaandika JANJARO kafukuzwa Shule Mara Janjaro Kafeli Mara Janjaro kaacha Shule ikiwa sasa Hawawezi kuiendesha Mitandao yao katika habari za Uhakika waache Wasijihusishe na kazi za habari nakumbuka nikiwa katika Tour yangu ya South Africa MILLARD AYO Alifanikiwa kunipigia Cm nikiwa Nje ya Tanzania anaefanya kazi katika Ofisi ya CLOUDS MEDIA GROUP alinipigia cm na kunifanyia Mahojiano kwahiyo nilifurah sana nikaona anaithamini kazi yake hapendi kutangaza kitu kisichokuwa na uhakika ANAPITA Anaefanya kazi katika EA RADIO kipindi cha POWE JAMES tunachat na kuwasiliana katika BBM pia Huwa Atangazi kitu bila kuniuliza na DJ CHOKA MR APPITITE pia aweki kitu kwa Blog yake bila kuniuliza hawa ndio nliokua nikiwasiliana nao nikiwa Safari, Tafauti na Hao, watakaoandika habari Totauti isiyofanana na hao nnaowasiliana nao juweni hao ni waongo ni wavivu wa kutafuta habari Wasiwapotoshe Watanzania ninaOmba kuzungumza Neno la mwisho.. Mimi Abdul-Aziz Abubakari Chende Ninae julikana kwa jina la JANJARO SIJAFUKUZWA SHULE,WALA SIJAACHA SHULE,NAWALA SIJAFELI na NIPO KIDATO CHa TATU...Form III ndio DARASA LANGU NA NDIO MAANA NIMEWEZA KUANDIKA NYIMBO YA MAISHA YA SKONGA na Najua itamgusa Kila Mwanafunzi ,Ikiwa Safari yangu ya Kwenda SOUTH AFRICA IMEWAUMA BASI FAHAMUNI YA KWAMBA nimejifunza MENGI katika SAFARI YANGU Kwanza imenifanya nizidi kujua mziki zaidi pili imenifanya nijue kufanya show za kiInternational tatu imenifanya nikutane na Mastar wengi wakanifahamu tukabadilishana Contact.. Wakasikiza kazi zangu na kuwa na Connection nao hivyo naomba mtambue mziki pia ni moja ya Maisha yangu ni kama vile nna miguu miwili shule mguu wa kwanza mziki mguu wa pili hivyo siwez kukata wowote katika iyo miguu miwili... AMEEN..napenda Shule napenda mziki,Narudia tena Napenda Shule napenda mzik...NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNISAIDIA KUFIKA HAPA.. Naishukuru COMPANY YANGU YA MTANASHATI/OSTAZ JUMA.../Nawapenda WATANZANIA

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ