MCHEZAJI MKONGWE WA LIVERPOOL, JAMIE CARRAGHER KUSTAAFU MWISHO WA MSIMU
Posted in Jammie Carragher, Liverpool
BEKI MKONGWE wa Liverpool Jamie Carragher ametangaza kuwa atastaafu Soka mwishoni mwa Msimu huu baada ya kuichezea Klabu yake zaidi ya Mechi 700 na kushika Rekodi ya kuwa Mtu wa pili, nyuma ya Ian Callaghan, kwa kucheza Anfield Mechi nyingi zaidi.
Carragher, mwenye Miaka 35 na ambae ameichezea England mara 38, alijiunga na Timu ya Vijana ya Liverpool akiwa na Miaka 9 na kuanza kuichezea Timu ya Kwanza Januari 1997 dhidi ya Middlesbrough.
Carragher alikuwemo kwenye Kikosi cha Liverpool kilichotwaa UEFA CUP Mwaka 2001 na UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2005 na vile vile ameshatwaa FA CUP mara 2 na Kombe la Ligi mara 3.
0 Maoni/comments: