Thursday, February 7, 2013

0

CHELSEA NA MAN-UNITED ZATANGAZA ZIARA ZA MWISHO WA MSIMU

Posted in ,
>>CHELSEA KUZURU THAILAND, MALAYSIA & INDONESIA
>>MENEJA KWA ZIARA YA CHELSEA HAJULIKANI!!
>>MAN UNITED WATAZURU AUSTRALIA, HONG KONG & JAPAN
WAKATI Klabu za Chelsea na Manchester United zikitangaza Ratiba zao za Ziara zao kujisuka kwa ajili ya Msimu mpya wa 2013/14, Mchezaji Mkongwe wa Liverpool, Jamie Carragher, ametangaza kustaafu Soka mwishoni mwa Msimu huu.
CHELSEA YATANGAZA TRIPU YA THAILAND, MALAYSIA NA INDONESIA
Chelsea wametangaza kuwa watacheza Mechi Nchini Thailand, Malaysia na Indonesia ikiwa ni Ziara yao ya Mwaka 2013 kabla kuanza Msimu mpya wa 2013/14.
Mwaka 2011, kabla Msimu mpya kuanza, Chelsea walitembelea Bara la Asia na kwenye Msimu huo mpya wa 2011/12 wakatwaa Ubingwa wa Ulaya na FA CUP.

++RATIBA CHINI>>

ZIARA 2013>>RATIBA ya CHELSEA:
Thailand
Singha Thailand All-Star XI v Chelsea [Singha Cup]
Bangkok, Thailand Julai 17
Malaysia
Malaysia X1 v Chelsea
Kuala Lumpur, Malaysia Julai 21
Indonesia
Indonesian X1 v Chelsea
Gelora Bung Karno Stadium, Jakarta, Indonesia Julai 25
---------------------------------------------------------------------
Mbali ya kuthibitisha Ziara hii, Klabu ya Chelsea haijatangaza Timu yao itakuwa chini ya Meneja gani kwani Mkataba wa Meneja wa sasa, Rafael Benitez, ni hadi mwishoni mwa Msimu huu.
MAN UNITED KUZURU AUSTRALIA, HONG KONG & JAPAN
Manchester United, ambao walishatangaza mapema kuzuru na kucheza Mechi huko Australia, Hong Kong na Japan, pia wametangaza kuongeza Mechi moja Nchini Japan ambayo watacheza na Klabu ya Cerezo Osaka, Klabu ambayo Mchezaji wa Man United, Shinji Kagawa, alianzia Soka lake la kulipwa kabla kuhamia Borussia Dortmund ya Ujerumani.
---------------------------------------------------------------------
ZIARA 2013>>RATIBA ya MAN UNITED:
Australia
Australian A-League All Stars v Manchester United
Jumamosi Julai 20, ANZ Stadium, Sydney
Hong Kong
Kitchee FC v Manchester United
Jumatatu Julai 29, Hong Kong Stadium
Yokohama & Osaka, Japan
Yokohama F·Marinos v Manchester United
Jumanne Julai 23, Nissan Stadium
Cerezo Osaka v Manchester United
Ijumaa Julai 26, Osaka Nagai Stadium
---------------------------------------------------------------------------------
Tangu wamnunue Shinji Kagawa wa Japan, Manchester United wamezidi kupendwa Nchini humo na kuzoa Mashabiki wengi mno.
Mtendaji Mkuu wa Man United, David Gill, akielezea Ziara hiyo alisema: “Man United ilianza kutembelea Japan Miaka 20 iliyopita na Mashabiki wetu Siku zote wameonyesha sapoti kubwa.”
Nae Rais wa Cerezo Osaka, Masao Okano, amesema: "Klabu yetu Cerezo na Mji wa Osaka ina furaha kucheza Mechi na Manchester United hapa Osaka.”

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ