ANAYESHIKILIA REKODI YA MABAO SI MESSI, NI CHITALU: ZAMBIA FA WANENA
Posted in Chitalu, Lionel Messi, Zambia FA
Kutoka SokaInBongo.com
>>WADAI CHITALU NDIE MFUNGAJI BAO NYINGI, 107 MWAKA 1972!
Chama cha Soka cha Zambia, ZFA, kimedai
kuwa Straika wao Godfrey Chitalu ndie anaeshikilia Rekodi ya kufunga
Bao nyingi ndani ya Mwaka mmoja wa Kalenda na si Lionel Messi kama
inavyoshabikiwa.
Wikiendi iliyopita, Messi alifunga Bao
lake la 86 kwa Mwaka 2012 na kuipiku Rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na
Mjerumani Gerd Muller alipofunga Mabao 85 Mwaka 1972 lakini sasa Zambia
wameibuka na kudai Rekodi hiyo ya Goli nyingi bado inashikiliwa na
Godfrey Chitalu aliyoiweka Mwaka 1972 kwa kufunga Bao 107 wakati
akiichezea Kabwe Warriors na Timu ya Taifa ya Zambia.
Msemaji wa ZFA amedai: “Tunayo Rekodi hii, imerekodiwa Zambia lakini, bahati mbaya, haikurekodiwa Dunia nzima!”
ZFA imesema kuwa sasa wameunda Tume huru
kuihakiki Rekodi ya Chitalu kuonyesha kila Mechi aliyofunga Goli na
matokeo ya Tume hiyo yatatumwa CAF na FIFA ili wadhihirishe ukweli wa
madai yao.
Godfrey Chitalu alifariki Mwaka 1993 kwenye Ajali ya Ndege iliyowaua pia Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zambia huko Nchini Gabon.
0 Maoni/comments: