Sababu Za Jamaica Kukimbiza Mwenge Vyema katika Olympics
Posted in
London Olympics 2012
Kwanini
Jamaica imeshikilia usukani wa riadha na mbio fupi?kwanini wao ndo
wanaongoza kwa sasa duniani?Asafa Powell,Usain Bolt,Blake..kwa wanawake
Shelly-Ann Fraser-Pryce anatetea taji lake la mita 100,huku Veronica
Campbell-Brown akitetea ya mita 200
Ushakaa chini ukafikiria
kwenye msatri wamejiandaa kukimbiza upepo then unakuta wajamaica
watatu.kijana mdogo Yohan Blake,Usain Bolt na veteran Asafa Powell??
Yaani ni kukimbizana kama vichaa..sasa ngoja nikupe hii,kwanini hawa
wajamaica wanaongoza kwa kukimbiza upepo duniani,sio wanawake wala
wanaume..yaani wote ni balaa.Kabala ya yote tukubaliane kuwa kwenye mbio
za kupokezana vijiti Jamaica wanashinda,hamana wa kuwazuia,yaani kijiti
kipokelewe na Powel aende kumpa Blake halafu blake ampe Bolt??hawa
washapita kweny hizo!!
Mimi nataka tucheki sababu za wao kuongoza dunia ya wakata upepo.
1.Role models(kioo cha jamii)
Hawa watu tunawaita vioo vya jamii,yaani jamii inawaangalia ndo ijue
nini cha kufanya,jinsi ya kufanya na wakati gani wa kufanya.
Ulimwengu wa technolojia ndo umefanya Bolt asikike sana pengine kuliko
wajamaica wenzake waliopita hapo zamani.Lakini ukweli ni kuwa hakuamka
na kuanza kukimbia,alikua na role model wake! Bolt hata yeye mwenyewe
alishawahi kukiri na kusema,kwa yeye kufika hapo alipo ilibidi awe ana
ndoto za kufanya alichokuwa anafanya gwiji wa mbio za mita 200 za
Olympic na mshindi mara 6 wa mashindano ya Jumuiya ya madola, Don Quarie
(Jamaican).
Hata kwenye mashindano ya mwaka jana Daegu,Usain
Bolt alivyotolewa kwa kufanya foul wakati wa kuanza,kijana aliyeshinda
mita 100 ni Yohan Blake amabaye naye anakiri role model wake ni Usain
Bolt.
Kwa upande wa wanawake,Campbell-Brown alikuwa chini ya
uangalizi wa gwiji mwingine Merlene Ottey,Ottey mwanamama aliyeweka
record ya kushinda medali 14 kwenye mbio fupi za mita 100 na bado
alikuwa anashindana akiwa na umri wa miaka 50!!!!!!!!!!!!
2.Hard Schools (shule zenye mazingira magumu)
Campbell na Ottey wote wamepitia shule moja,Vere Technical(jina la shule).
Mazingira ya maeneno kama hayo ukichanganya na mashindano yanayofanyika
kila mwaka Jamaica yanayoitwa Boys and Girls championships ndo
yanafanya hawa watu wanajengeka kimichezo na morale inakuwa juu kupita
maelezo.
Campbell anasema alivyokuwa bado shule ya primary walimu
wake walimwambia ''Una kipaji sana,na shule pekee itakayoweza kulinda na
kukuza ulichonacho ni Vere Technical'' na hadi leo Vere imekuwa
chimbuko la kutoa wakimbiza upepo bora Jamaica.
3.Cultural Factors(sababu za kiutamaduni)
Umaskini wa Jamica kama nchi ni sehemu ya utamaduni wao(hahahaha).
Bolt na Campbell wamekulia katika eneo moja,Trelawny.Wanasema kulikuwa
hamna maji nyumbani,kitendo cha wao kufuata maji kilometa kadhaa kila
siku,hasa eneo lenye milima ilikuwa ni part ya amzoezi yaliyowatengeneza
mwili na kuwatayarisha waje kuwa bora.
Yohan Blake anasema
kuishi Jamaica kunafurahisha sana,unaishi na wanyama kama rafiki
zako,anasema yey kuchinga mbuzi na kuanza kukimbizana nao ni part ya
mazoezi yaliyomtayarisha na kuwa hivi alivyo sasa.
4.Sprinting Show-off (mbio za kutengeneza status na jina,kujionyesha)
Jamaica hiki ni kitu cha kawaida sana,wakati nchi nyingine wao
wakifanyiana masifa mtaani na magari ya baba zao,kushindana nguo mlimani
city na kumwaga pesa club..
Jamaica wao ni kukata upepo,tena kama
wanawake wapo hapo ndo utakimbizana hata na risasi,vitu kama hivi ni vya
kawaida sana mitaani Jamaica,na vina mchango mkubwa sana katika
mafanikio yao hadi walipofikia.
PS.
Nimeandaa kwa msaada wa kipindi cha CNN
Aiming For Gold Show kilichorushwa June 24 1630 GMT
0 Maoni/comments: