Arsenal Win Game In Malaysia
Posted in ArsenalArsenal, iliyogubikwa na wingu zito la utata kuhusu hatima ya Nahodha wao Robin van Persie anaetaka kuhama, leo imeanza Ziara yake Barani Asia ya kujifua kwa ajili ya Msimu mpya Nchini Malaysia kwa ushindi wa mwishoni wa bao 2-1 dhidi ya Kombaini ya Malaysia na wakati huo huo kuna habari toka Makao Makuu yao zikithibitisha kuwa Sentahafu wao Laurent Koscielny amesaini Mkataba mpya wa muda mrefu na pia Klabu hiyo imefikia makubaliano ya kumchukua Winga kutoka Klabu ya Malaga, Santi Cazorla.
Huko Uwanja wa Taifa, Bukit Jalil,
Arsenal, iliyokuwa na Chipukizi wengi, ilijikuta iko nyuma kwa bao 1-0
baada ya Mohd Azmi Muslim kufunga kwa shuti la mbali katika Dakika ya 45
lakini wakasawazisha kwenye Dakika ya 86 kupitia Kiungo toka Germany
Thomas Eisfeld, Miaka 19, na kupata bao la pili na la ushindi alilofunga
Chuks Aneke.
Arsenal sasa wanaelekea Beijing ambako Ijumaa Julai 27 watacheza na Mabingwa wa England Manchester City.
Laurent Koscielny akubali Mkataba mpya wa muda mrefu
Sentahafu wa Arsenal Laurent Koscielny amekubali kusaini Mkataba mpya wa muda mrefu kwa mujibu wa Tovuti ya Arsenal.
Koscielny, Miaka 26, alijiunga na
Arsenal Mwaka 2010 akitokea Klabu ya Ufaransa Lorient na amekuwa
Mchezaji wa kuaminika wa Timu hiyo akianza Mechi 85 kwa Arsenal katika
Miaka miwili iliyopita na hizo ni Mechi nyingi kupita Mchezaji yeyote
mwingine wa Arsenal.
Mwaka jana, Koscielny aliitwa kuichezea
France kwa mara ya kwanza na tangu wakati huo ameshaichezea France mara 4
na mara ya mwisho ilikuwa ni Mwezi Juni kwenye Robo Fainali ya EURO
2012 walipofungwa 2-0 na Spain.
Arsenal yakubaliana na Malaga kumchukua Winga Santi Cazorla
Huku kukiwa na wingu zito kuhusu hatima
ya Nahodha wao Robin van Persie ambae amegoma kusaini Mkataba mpya
wakati wa sasa ukiwa umebakisha Miezi 12 tu na akivumishwa kuhama,
taarifa ndani ya Arsenal zimedai Klabu hiyo imefikia makubaliano na
Malaga ili kumchukua Winga Santi Cazorla kwa dau la Euro Milioni 20
(£15.6m).
Hadi sasa Arsenal imeshapata Wachezaji
wapya wawili ambao ni Mastraika Olivier Giroud kutoka Montpellier na
Lukas Podoloski kutoka Cologne.
Source: sokainbongo.com
0 Maoni/comments: