KOMBE la DUNIA-Brazil 2014: RAIS Brazil asaini Sheria Bia kuuzwa kwenye Mechi
Posted in World Cup 2014 Brazil
Rais
wa Brazil Dilma Rousseff amesaini Sheria inayoruhusu Bia kuuzwa kwenye
Mechi wakati wa Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Nchini humo
Mwaka 2014 baada ya Muswaada wa Sheria hiyo kupitishwa Bungeni Mwezi
uliopita licha ya kupingwa sana.
Tangu Mwaka jana kumekuwa na mvutano
mkubwa kati ya FIFA na na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Brazil ambao
walikuwa wakichangia Muswada wa kupitisha Sheria ya Kombe la Dunia ambao
moja ya vipengele vyake ni kuruhusu uuzwaji wa Bia kwenye Viwanja
vitakavyochezwa mechi za Kombe la Dunia.
Tangu Mwaka 2003 uuzwaji wa Pombe kwenye
Viwanja vya Soka ulipigwa marufuku ili kuzuia fujo lakini moja ya
masharti ya FIFA ni kuruhusu Pombe Uwanjani kwa vile baadhi ya Wadhamini
wake wakubwa, kama vile Budweiser, ni Watengenezaji Bia.
Muswada huo wa Kombe la Dunia ulikuwa
upigiwe kura mwishoni mwa Mwaka jana lakini ulichelewa kutokana na
mvutano wa kuruhusu Bia huku Waziri wa Afya wa Brazil, Alexandre
Padilha, akiwa ndie mpinzani mkubwa wa kuruhusu kuuzwa kwa Pombe
Viwanjani.
Sheria ya Kombe la Dunia iliyosainiwa na
Rais Dilma Rousseff haitaji lolote kuhusu kuzuiwa uuzwaji Bia hivyo
kuacha nafasi Bia kuuzwa wakati wa Mechi lakini Wachunguzi wamedai
baadhi ya Majimbo ya Brazil yana Sheria zao zilizo wazi kupinga uuzwaji
Bia na hivyo wanaweza kuamua kuendelea kupiga marufuku Bia.
Source: sokainbongo.com
0 Maoni/comments: