Wednesday, June 13, 2012

0

AY na Sauti Sol Kwa pamoja wiki hii ndani ya BBA

Posted in , , ,

Huu ni mwaka wa Afrika Mashariki kushine! Na by the way sijui nchi zingine zinajisikiaje juu ya hili? Je! Big Brother Africa mwaka huu inataka kulitumia jukwaa lake kuutangaza muziki wa Afrika Mashariki ili kuunyanyua zaidi labda pengine tuwe sawa na Nigeria na Afrika Kusini, ama muziki wetu ‘unabamba sana’!!!
Manaake imekuwa bandika bandua (which is good by the way, we no lie!!). Walianza Campmulla, akaenda Diamond, wiki iliyopita alienda Maurice Kirya na kwenye ‘wheels of steel’ akasimama the cutest female DJ alive in Africa!! (kwani uongo?) Dj Fetty mwenyewe! Mtoto akapiga ‘mikuno’ ya adabu Afrika ikampa salute.
Na sasa hivi it’s all over the media, kwamba Ambwene ‘AY’ Yesaya na bendi machachari ya ‘masela’ tupu ya Sauti Sol ‘watakinukisha’ wiki hii mjengoni! And guess what! Jamaa wanangoma ya pamoja tayari, ‘I dont wanna be alone (shukuru)’ ambayo AY aliwashirikisha.
Huenda hii ikawa ni sababu kubwa ya kuwapandisha wote kwenye stage wiki hii, si unajua zile style za kupiga ndege wawili kwa jiwe moja which at the end of the day it’s all good na waafrika wanaburudika.
So swali letu ni kuwa, I don’t wanna be alone ndio miongoni mwa nyimbo watakazoperform? What do you think, unadhani ni wimbo mahsusi kwa stage ya Big Brother ambayo mara nyingi inapendelea mizuka zaidi? Kwa ufahamu wetu wimbo huu ni wa kusikiliza zaidi. Ama ni aina ya nyimbo ambazo msanii ataziimba kwenye VIP concerts.
Concerts za watu wakubwa kama mameneja ama CEOs ambao wametoka out na wake/waume/wachumba/familia zao na hivyo hawapendi show za mizuka saaaana! Hawataki kelele nyingi zaidi ya kula bata kwa raha zao.
Lakini tunahisi AY na Sauti Sol wanalijua hili kutokana na tweet hii ya Sauti Sol iliyoandikwa juzi usiku, “So were @ the studio making a halflive track for our #BigBrotherStargame set. Its sounding massive hope @AyTanzania feels it. #Shukuru.”
By reading between the lines, utagundua kuwa jamaa wametengeneza live version ya Shukuru na kisha kumtumia AY aifanyie ‘tizi’!! Matumaini yetu ni kuwa wameichangamsha zaidi, ngoja tusubiri.
Kupata show hii kwa AY tunadhani imemfanya ‘the happiest dude alive on earth right now’. Kwanini? Ni kwasababu wiki hii pia video yake aliyoifanya mwishoni mwa mwezi uliopita huko huko Johannesburg Afrika Kusini inatoka.
“My videooooo PARTY ZONE Feat @Marcochali waaah sio Another Chapter ni ANOTHER BOOK,” alitweet wiki hii.
Japo hatujui kama itatoka mapema kabla ya yeye kwenda huko lakini ana uhakika sasa wa kurudi nayo mkononi atokapo huko! And tell you what! Mchongo huo umempa uhakika wa kufanya video nyingine ya mkwanja mrefu.
“AyTanzania Kuperform BBA j’pili, anaangalia uwezekano wa kuitumia hiyo nafasi kufanya video nyingine ya Milioni 30” (Amplifaya). Naona ule msemo wa ‘money make money’ umemuingia vema Ambwene. Go and chop that money homeboy!!!
Mwisho, ni matumaini yetu kuwa Prezzo ataenjoy sana kukutana uso kwa uso na mshikaji wake AY. Hatupati picha kama Biggie akimruhusu mfalme wa bling apande stejini na kuimba ‘Nipe nikupe, raha tupate’ along side AY! Hapatosha zaidi ya fireeee kwenye stage.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ