Thursday, June 20, 2013

0
Jun 2013 20

WASANII AMBAO SIO MFANO WA KUIGWA NA JAMII ( WASOME HAPA)

Posted in , ,
Mastaa wanaotikisa dunia, akiwepo Miley Cyrus, mwanamama Kim Kardashian pia Chris Brown wametokea katika nafasi ya juu kabisa katika orodha ya watu maarufu ambao kwa kulingana na mienendo yao, si mfano mzuri wa kuigwa na jamii hasa watoto ambao hupotezwa kwa kiasi kikubwa na matendo yao.



Hii ni kwa mujibu wa kura za wazazi kwa njia ya mtandao mmoja maarufu huko Marekani ambao pia ndani yake kuna wasanii kama Kanye West, Lil Wayne na Justin Bieber, ambao kura za wazazi wengi walioshiriki katika zoezi hili zinaonyesha tofauti ya asilimia chache kati yao.

Orodha hii pia imezingatia kuangalia sababu za wazazi hawa kuwaweka wasanii hawa katika kundi hili, ambapo matumizi ya mihadarati ama bangi, lugha chafu, matendo ya vurugu ni kati ya sababu kubwa ambazo zimewafanya wasiwe mfano mzuri wa kuigwa.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ