Sunday, December 30, 2012

0

YALIYOJIRI 2012 KATIKA SANAA YA MUZIKI BONGO

Posted in , , , , , , ,

Muziki wa bogno umepiga hatua kubwa sana hasa katika mwaka huu. Mengi Yametokea, Vipaji vingi vimejitokeza. Mitindo mingi ya Kimziki na Dansi iliongezeka.

1. Kupaa Kwa Ommy Dimpoz
Pooooz kwa Poz...
Ommy Dimpoz Na Vanessa Mdee
Huu ulikua ni mwaka wa kijana huyu ambaye alianza kwa kutoka na Nyimbo NAI NAI iliyompa tuzo za kili kwa kumshirikisha Ally Kiba, Akaja na BAADAE, na baadae akafunga mwaka kwa nyimbo ya  ME & YOU ft. Vanessa Mdee. Kijana huyu ameepata mafanikio mengi na kupiga hatua moja ikiwa ni kufanya video nchini Afrika Kusini. Kijana huyu pia alitoa malalamiko ya kumshutumu Lord Eyez kuiba PowerWindow za Gari Lake(Rav4).



2. Kuendelea Kuvuma kwa WEUSI.
WEUSI ni Kundi Muanganiko wa wasanii wa Arusha toka kundi la N2N na RiverCamp likijumuisha Wasanii kama Lord Eyez, Joh Makini, G-Nako, Nikki Wa pili na Bonta. Kundi hili limekua na mafanikio mengi huku kashfa aliyoipata Lord Eyez, kulifanya lipate sifa mbaya na wale walioamini hilo.






3. Udhamini wa OSTAZ JUMA NAMUSOMA kwa WATANASHATI
Watanashati wamevuma sana katika mwaka huu, Wamemrudisha PnC katika Fani, Wameokoa kipaji cha Dogo Janja, Suma Mnazaleti kwa udhamini mzuri walionao. Kundi hilo lilizidi kuwa kubwa kadri mda ulivyokwenda, na wamevuma zaidi kwa nyimbo zao. Uwepo wa Marehemu Sharo Millionea na Teja Kitale uliweka uamsho katika kundi.
HONGERA OSTAZ JUMA




Mengineyo
  • Ferooz Arudi na "ndege mtini"
  • Solo Thang "Miss Tanzani"
  • Shilole Atoka Kimuziki Zaidi
  • Vanessa Mdee Na Tasnia Ya Muziki.
  • Hakuna Kama Diamond, Akimbiza Sana katika Tasnia Hii
  • UJIO WA RICK ROSS-FIESTA
4. Ujio Wa PAH-ONE
Pah-One ni kundi la muziki linalofanya kazi zao kupitia HOME TOWN RECORDS chini ya Nahreel Mkono na kaka yake Thomas Mkono. Kundi hili linaundwa na wasanii wanne. NahReel, Ola, Damas na 1st Lady AIKA. Kundi hili limepata mafanikio hasa baada ya kuvutia mashabiki wengi kwa style yao ya muziki, mavazi na jinsi wanavyofanya video zao. Nyimbo zao zilizovuma, Asambeni, YOU, Ghetto, I wanna Get Paid(IWGP).

Kupaa Kwa Vichwa vipya vya Hip Hop Vipya
  • Stamina
  • Tash
  • CountryBoy
  • Baghdad
  • Mabeste

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ