Next
Previous
Showing posts with label LANGA. Show all posts

Monday, September 30, 2013

0

NIKKI MBISHI KAACHIA MIXTAPE MPYA AMBAYO KAWAENZI LANGA NA NGWAIR | TRACK LIST NA COVER

Posted in , ,


Nikki Mbishi ameachia final cover pamoja na mtiririko wa nyimbo zitakazokuwa kwenye malcom xi mixtape. Kwa Tsh 5000 tu utaweza kupata Malcom XI mixtape ndani kukiwa na wasinii kibao kama Farzhaad ‘Invincible’ Bandali, Jordan Kalyembe, KalApina Kikosi Cha Mizinga, Mycle Bertold, Malcolm Nikki Mbishi Jr., Harry Kaale, Niite Songa, Nikki Mbishi BabaMalcom, Minah Madoido and P The-mc Polymath.

Ndani ya mixtape hiyo kutakuwa na wimbo unaitwa Langa na Mangwea ambao Nikki Mbishi amewaenzi wasanii hao wakali walipoteza maisa mwaka huu

Mtiririko wa nyimbo (tracklist) ya malcom xi mixtape ni kama ifuatavyo

1: intro

2: a.k.a

3: Nay Wa Mitego

4: yote sawa

Wednesday, June 19, 2013

0

HII NDO BARUA YA ZOLA D, KWENDA KWA WALIOHUDHURIA MSIBA WA MANGWAIR NA LANGA KILEO (SAFI SANA)

Posted in , ,
BARUA MAALUM KUTOKA KWA DAVID MICHAEL MLOPE,aka ZOLA D KWENDA KWA WATANZANIA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA MSIBA WA MANGWEAR.pamoJa na LANGA KILEO.



DAVID MICHAEL MLOPE BOX 70098 DAR ES LAAM TANZANIA.
PHONE +255715296889.
barua no 2.

naendelea pale nilipoishia kwenye barua ya mwanzo namba 1 ...... habari zenu ndugu zangu watanzania hope wote ni wazima na mnaendelea na mishe za maisha mimi mzima siJambo Japo nina stress nyingi sana mpaka nimepungua kg 3,kutokana na mawazo na kuto kulala tokea msiba wa arbert mangwear pia tumepata pigo Jingine la mdogo wetu langa kileo,siJui niseme nini kwa Jinsi inavyo niuma ila nina mwachia Mungu maana ndio kazi yake pia pole sana wazazi wa langa kileo baba na mama pamoJa na familia yote kwa uJumla pia asante sana watanzania wote walioJitokeza kwenye safari ya kumsindikiza ndugu yetu msanii mwenzetu langa kileo leo nataka kugusia sana upande wa maisha yetu na dini kama binadamu tunaopita tu kwenye hii dunia maana kila mtu atakufa vitabu vya dini vimeandika.Ndugu zangu wapendwa watanzania dunia imekwisha ndugu zangu tuanze kufanya ibada na kutenda yaliyo mema coz free masons wanawatumia ndugu zetu kwenye big brother na seemu mbali mbali kuwaonyesha wakiwa watupu uchi na kuwadanganya kwa pesa,na sasa wameingia africa mashariki kwa kishindo sana hawa free masons Juzi tu nimepigiwa simu na watu kampuni Jina siri yangu wanataka nikacheze video ya ngono na mwanamke kwa kitita cha milion 70 nikawaeleza siwezi kufanya uchafu kama huo,na leo tena wamenipigia wakisema watanipa milion 100 bado nimekataa Je unaelewa kwa nini nimekataa? free masons wanataka viJana shupavu na wenye akili na vipaJi ili waweze kuwatumia kuitangaza dini yao na wanaweza kukupa maisha ya Juu kwa gharama yoyote ile,

Sunday, June 16, 2013

0

Various Artists --" GOODBYE " (New Tribute Music Video For Langa)

Posted in , ,

|| A tribute music video I did for my late friend Langa. Featured Varios Artists. I did finish the music video for a total of 16 hours. ( 4 hours of shooting plus 12 consecutive hours of editing...) ||-Maneno ya Director Mushalla

Artists : Various Artists
Track : Goodye
Prod. : Christon/NK productios
Filmed, Edited & Directed By Jerry Mushala

Saturday, June 15, 2013

0

IN MEMORY OF LANGA KILEO | WASIFU WA MAREHEMU (VIDEO ZA NYIMBO ZAKE NA BAADHI YA PICHA)

Posted in


Juzi alhamisi jioni tulipata taarifa juu ya kifo cha msanii wa hip hop ex-member wa wakilisha. Ni mtaalamu na mwanamuziki stadi wa Hip Hop nchini aliyeweka wazi kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.

 Ili kuonyesha anachukizwa, Langa alilieleza jarida moja la burudani kwamba anakusudia kuanzisha Taasisi ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya.

Alisema matumizi ya dawa hizo yaliathiri shughuli zake za muziki na hakuwa na jambo lolote endelevu katika muziki wake.

Kimuziki Langa alianzia kundi la Wakilisha akiwa na Witness Mwaijega na Sarah Kaisi, ambapo walikuwa washiriki wa mashindano ya muziki ya Cocacola Pop stars, yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Wakiwa na kundi hilo walifanikiwa kufyatua kibao cha ‘Hoi’, ambacho kiliteka wapenzi wa muziki.

Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness walifyatua kibao cha ‘No Chorus’.


Baada ya hapo Langa alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’ ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha.

Hata hivyo Langa alionyesha yeye ni bora na ana kipaji cha muziki. Amekuwa shujaa kwa kuendesha kampeni kali za kupinga matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana. Serikali inapaswa kusaidia juhudi zake pamoja.

Huyu ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha.  Mbali ya Langa, wengine ni Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwaijaga `Witness’. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kung’ara kisanii kwa wakali hao, ingawa kwa sasa kundi hilo limesambaratika, kila mmoja akitamba kivyake.

Lakini kwa bahati mbaya, mmoja wao, Langa kwa miaka ya hivi karibuni hakusikika kabisa, jambo lililomlazimu mwandishi wa makala haya kumtafuta sababu za ukimya wake.


Haikuwa kazi rahisi, lakini hatimaye Langa alipatikana na bila kutafuna maneno alisema kwamba, alishindwa kufanya kazi baada ya kuwa `teja’ aliyekubuhu.

Yaani alizama katika matumizi ya dawa za kulevya kiasi cha kupoteza kabisa mwelekeo si wa kisanii pekee, bali hata kimaisha.

“Siyo siri, kilichokuwa kimenifikisha katika hali hiyo ni dawa za kulevya. Kwa miaka mitano nilitumia sana Cocaine, Heroin, bangi na pombe. Namshukuru Mungu sasa nimerejea katika hali yangu.

“Siamini kama nimenusurika kwa sababu madawa yalinitesa, nikafanya mengi ya ajabu yaliyoichukiza familia yangu na marafiki ikiwa pamoja na kuwa mwizi na mkabaji mitaani na nyakati za usiku,” anasema Langa ambaye kundi lao la Wakilisha lilitamba na nyimbo kama `Unaniacha Hoi’ na `Kiswanglish’.

Anaeleza kwamba, kwake hayo ndiyo aliyoyaona maisha yanayomfaa, akidai awali alikuwa amechoshwa kuishi kwa masharti kutoka kwa wazazi wake waliokuwa wanampa mwongozo wa maisha, lakini bila kujua akadhani `anachungwa’.

Kwamba, umaarufu na ngekewa ya kuzishika pesa katika umri mdogo kupitia muziki vilimtia kiburi zaidi, na hivyo kuamua kujitenga kabisa na familia yake iliyomlea kwa mapenzi mazito.

“Niliamini naweza kujitegemea kupitia kazi yangu ya muziki, nikajichanganya mtaani,” anasema kijana huyo aliyetoa kibao chake cha kwanza, Matawi ya Juu mara baada ya kusambaratika kwa kundi la Wakilisha kutokana na kila mmoja kuamua kujitegemea kimuziki. Na kweli, Matawi ya Juu ilidhihirisha kuwa Langa ni moto wa kuotea mbali katika fani. Aliweza kusimama kwa miguu yake na kutikisa.

Mwenyewe anasema: “Jina hilo la Matawi ya Juu lilidhihirisha hivyo pale video ya kibao hicho ilipotajwa kuwania Tuzo za MTV Base kwa upande wa hapa Bongo miaka michache iliyopita, kisha kutwaa Tuzo ya Kisima nchini Kenya.

“Moto huo uliwafanya baadhi ya wasanii wakongwe katika gemu ya Bongo Fleva kunitafuta na kunipa majukumu ya kushiriki katika kazi zao, ikiwemo Chagua Moja ya Farid Kubanda `Fid Q’.

“Baada ya kuona wakongwe wamekubali vitu vyangu na kuanza kunishirikisha…nikapata pia safari za nje ya nchi. Huko Nairobi (Kenya) niliweza kufanya kazi na vichwa vikali vinavyounda Kundi la Necessary Noise, Naaziz na Wyre (Kevin Wyre).

Anasema mafanikio hayo yalimtuma kufyatua albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la Langa, akiamini itampaisha zaidi kimaisha na kimuziki. Hata hivyo, mambo yalikwenda kinyume. Anasema alipoipeleka sokoni, wauzaji wakubwa waliigomea, hivyo kumpa wakati mgumu wa kuwaza na hatimaye kujikuta akiongeza kasi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Siyo siri, kugoma kwa albamu yangu sokoni kulichangia kasi ya kutumia dawa za kulevya…niliona ni njia pekee ya kuondoa mawazo kwa sababu kazi iligoma, na home (nyumbani) nilishaharibu.

Sikufanya tena kazi kwa umakini na kila kazi niliyoitia haikufanya vizuri….” Anasema kwamba, baada ya mambo kumwendea mrama, ndipo alipoanza kuiba vitu nyumbani kwao kwa lengo la kuviuza na inapotokea amekosa, alidiriki hata kupiga debe katika vituo vya mabasi ili mradi apate fedha za kununua `unga’.

Haikuishia hapo, kwani anasema alijiingiza katika kundi la wahuni waliojihusisha na wizi na ujambazi. “Kwa ujumla nilipoteza mwelekeo. Maisha yangu yakawa ya kutembea na kisu kama kitendea kazi changu katika wizi,” anasema huku akitikisa kichwa kama ishara ya kujutia matendo aliyoyafanya kwa msukumo wa madawa ya kulevya. Anakumbuka akiwa mtumwa wa `unga’, aliingia katika mikasa kadhaa ikiwa pamoja na kupigana na polisi baada ya kunaswa na dawa hizo haramu.

Katika wizi, chochote alichokikuta mbele yake kilikuwa halali. Anasema alikwapua vitu magengeni, madukani na hata magari yaliyoegesha vibaya alinyofoa vioo na mashine zinazosaidia kupandisha na kushusha vioo ndani ya gari.

“Ni matukio ya aibu. Yanasikitisha…,” anasema Langa anayedokeza kwamba, akiwa mtumiaji wa `unga’, alikuwa anakutana na wasanii na watu wengine mashuhuri. Hata hivyo anakataa kuwataja, akidai ni siri yake. `Ufufuo’ wa Langa kutoka katika lindi la mateso ya dawa za kulevya ulipatikana kuanzia Machi mwaka huu, baada ya familia yake kumpeleka kijana wao kwa tiba maalumu ya kuachana na matumizi ya `madudu’ hayo. Na kweli, elimu imemwingia na kujikuta akirejea ufahamu wake wa kawaida.

Ametangaza kuachana na `unga’, pombe, sigara na badala yake amejikita zaidi katika mazoezi ya kurudisha mwili wake katika hali ya kawaida. Aidha, amekata shauri la kuirudia fani yake na tayari ana vitu vipya, Bombokiata na Mteja Aliyepata Nafuu.

Anasisitiza kwamba, kutokana na mateso aliyoyapata, anakusudia katika siku za baadaye afungue kituo chake cha tiba ya dawa za kulevya ili aweze kuwaokoa vijana wengine wanaoangamia kutokana na matumizi ya dawa hizo haramu zinazopigwa vita karibu kote duniani. “Nimenusurika, namshukuru Mungu.

Nami najipanga kutaka kuwasaidia wengine waachane na mateso ya dawa za kulevya. Pia nichukue fursa hii kuwaomba msamaha wote niliowakosea kwa namna moja ama nyingine wakati nikiwa `teja’,” anasema Langa, kijana mwenye umri wa miaka 25.

Je, historia ya maisha ya Langa ikoje? Anasema Desemba mwaka 1985 jijini Dar es Salaam akiwa tunda la wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo. Alisoma Shule ya Msingi Olympio na Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.

Huyo ndiye Langa Kileo msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye baada ya kulewa umaarufu na kujikita katika matumizi ya dawa za kulevya, ameibuka na kujutia `ujanja pori’, sasa akitaka kujiingiza katika kampeni ya kuwaokoa vijana wengine waliozama katika `unga’. Anakusudia pia kurudi darasani kujiendeleza na masomo ya elimu ya juu. Je, atafanikiwa? Kwa hakika, hili ni jambo la kusubiri na kuona.


Friday, June 14, 2013

0

LANGA KUZIKWA JUMATATU : RATIBA KAMILI YA MAZISHI

Posted in
Ratiba ya mazishi ya marehemu LANGA KILEO itakuwa kama ifuatavyo …. Msiba upo nyumbani kwa wazazi wa LANGA ambapo ni maeneo ya MIKOCHENI nyuma ya hospitali ya AAR ….



Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu, Saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburini Kinondoni kwa mazishi ambapo imepangwa itakuwa ni majira ya saa kumi alasiri …

R.I.P Langa Kileo …

Saturday, May 11, 2013

0

VIDEO TEASER: LANGA-RAFIKI WA KWELI

Posted in ,

LANGA is set kuachia video yake mpya ... Video hiyo itafahamika kama RAFIKI WA KWELI ...
The video will drop soon for your eyes ikiwa imeongozwa na director na JERRY MUSHALA wa JERRY MUSHALA STUDIOS ...
LANGA ameachia TEASER ya video hiyo, check kipande cha RAFIKI WA KWELI hapa chini :

Thursday, March 21, 2013

0

LANGA IS BAACK: BRAND NEW TRACK> Langa - AM SUPPLYING

Posted in


Baada ya kuwa kimya kidogo kwenye industry ya muziki sasa rapper Langa kutoka Regent Estate, Mikocheni ameamua kurudi tena na ngoma yake mpya.
Langa (@LangaKileo) ame-release track yake mpya inayoitwa ''AM SUPPLYING''.
L.A.N.G.A [Lyrical And Natural Gifted African] alifanya vizuri sana kipindi cha nyuma kidogo na ngoma zake kama MATAWI YA JUU, GANGSTA, PIPI YA KIJITI na nyinginezo baada ya kutoka katika kundi la Coca Cola Popstars, WAKILISHA akiwa na Witness pamoja na Shaa.
Sikiliza na Download track AM SUPPLYING hapa chini alafu utupie comment zako kuhusu the come back of Langa...










Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ