Friday, January 24, 2014

0

TAARIFA JUU YA RAISI WA BARCELONA KUJIUZULU

Posted in ,

Na taarifa ikufikie kwamba Rais wa club ya Barcelona Sandro Rosell amejiuzulu Urais wa club hiyo Alhamisi usiku (January 23 2014) baada ya kikao kizito na bodi ya club hiyo ambapo uamuzi alikuja kuutangaza mbele ya waandishi wa habari muda mfupi baadae.
.Uamuzi huu umekuja baada ya Mahakama kuamuru uchunguzi ufanyike kuhusu usajili wa mchezaji raia wa Brazil ambae alisajiliwa June 2013 kwa pound milioni 49 akitokea Santos, uchunguzi ufanyike kwa sababu ya lalamiko kwamba pesa iliyotumika kwa uhamisho huo ilikua zaidi ya €57m.
Akielezea kujiuzulu kwake Rosell amesema kwa kipindi kirefu yeye na familia yake wamekua na wakati mgumu kutokana na yaliyotokea ndio maana anataka kuwa huru huku akisisitiza kwamba kusainiwa kwa Neymar kuko sahihi.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ