HII NDO NYIMBO YA KOMBE LA DUNIA 2014 BRAZIL | MJUE MKALI ALIYEIIMBA (WORLD CUP 2014 ANTHEM)
Posted in David Correy, Fifa World Cup 2014, World Cup 2014 BrazilKwa wale wapenzi wa burudani, hasa kwenye upande wa kandanda huwa wanaburudika sana pale ladha ya mchezo huo unapoambatana na “tune” nzuri za muziki ambazo mdhamini mkuu wa Kombe la Dunia, Coca Cola huandaa…Zikiwa zimebakia siku chache kufikia ufunguzi rasmi wa mashindano ya kombe la dunia kwenye soka, mwakani, 2014, David Correy ndiye kijana aliyefanikiwa kupata bahati ya kurekodi nyimbo itakayotumika ulimwengu mzima kwenye fainali hizo zitakazoanza kutimua vumbi mwakani…“The World Is Ours” ndiyo jina la ngoma hiyo.
“Waving Flag” ni ngoma iliyotokea kupendwa sana,toka kwa rapper mwenye asili ya Somalia, K’naan, si tu kipindi mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2010 yalipokuwa yakiendelea nchini Afrika Kusini, bali hata mara baada ya mashindano hayo kuisha, mdundo huo uliendelea kufanya vizuri sababu ya vionjo vilivyotumika kuitengeneza…
David Correy |
“Mpaka sasa nimefanikiwa kutimiza ndoto kubwa mbili maishani mwangu, kukutana na mama yangu mzazi pamoja na hii ya kuweza kurekodi nyimbo na kampuni hii ya CocaCola” alisema Correy…Pata ladha ya ngoma iyo hapa chini
Kwa sasa, msanii huyu yupo nchini Kenya amabapo amepata mualiko wa kwenda kutumbuiza kibao hicho, na atakuwa nchini humo kwa muda wa siku tatu…
Coca cola 2014 FIFA World Cup Trophy Tour ikiwa inaendelea, ambapo kwa sasa kombe hilo lipo nchini Kenya, Correy anatarajia kuondoka Ijumaa, Novemba 29 ambapo atalisindikiza kombe hilo nchini Tanzania kama ratiba ya safari ya mzunguko wa kombe hilo inavyosema…Itakuwa ni mara ya tatu kwa kombe hili kutembelea Tanzania, ambapo mara ya mwisho lilitua nchini Novemba,2009 na kupokelewa na raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
0 Maoni/comments: