MESSI AWEKA UHASAMA PEMBENI NA KUIUNGA MKONO MADRID
Posted in Lionel Messi
NYOTA Lionel Messi amejitokeza kuiunga mkono Madrid katika azma yao ya kutaka kuwa Wenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Mwaka 2020.
Messi, ambae ni Mchezaji wa FC Barcelona, ameweka kando Uhasama wa Klabu yake na Real Madrid ili kuunga mkono Mji Mkuu wa Spain, Madrid, kuwa Wenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Mwaka 2020.
Akiwa huko kwao Buenos Aires, ambako ndiko uamuzi wa nani atakuwa Mwenyeji wa Olmpiki ya Mwaka 2020 utafanywa hapo Septemba 7 na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Messi alijitokeza akiwa amejigubika Bendera Nyeupe ya Madrid ili kuonyesha kuunga kwake mkono kampeni ya Jiji la Madrid.
Akiwa huko kwao akiwa na Timu ya Taifa ya Argentina, Messi alisema: “Nipo na Madrid 2020.”
Awali Wawakilishi wa Messi waliamua Mchezaji huyo asiunge mkono kampeni hiyo ya Madrid kugombea Michezo hiyo ya Olimpiki lakini ni wazi sasa hilo limebadilika na Messi ameamua kuwa pamoja na Madridistas.
Kwenye uteuzi wa nani Mwenyeji, Madrid inashindana na Tokyo na Instabul ili kuwa Mwenyeji wa Mashindano ya 42 ya Michezo ya Olimpiki.

0 Maoni/comments: