KOCHA MKUU WA BARCELONA; TITO TILANOVA AJIUZULU KUFUNDISHA SOKA
Posted in FC Barcelona, Tito Tilanova
Muda mchache uliopita Rais wa Klabu ya Barcelona Sandro Rosell na Makamu wake Adoni Zubizareta wametangaza rasmi kuachana na huduma ya Kocha wao kipenzi Tito Tilanova kwa ajili ya matatizo ya Kansa.
“Tito Tilanova amejiuzulu kutokana na matatizo ya kansa” ndio imesikika kutoka kwa Sandro Rosell mbele ya mkutano na waandishi habari muda mchache uliopita
Sandro Rosell amesema ni huzuni kuondokewa na Kocha huyo kwa sasa lakini wanamtakia matibabu mema na afya njema
Tito Vilanova(44) amefikia uamuzi huo baada ya kufanyiwa vipimo vya afya ambapo imegundulika kuwa tatizo lake la saratani ya tezi zilizoko kooni mwake limejirudia tena na anatarajiwa kwenda nchini Marekani kupewa matibabu ya kitaalamu zaidi .
Tito Vilanova aligundulika kuwa na tatizo hilo miaka mitatu iliyopita ambapo alifanyiwa upasuaji na ilidhaniwa kuwa amepona kabisa kabla ya tatizo hilo kujitokeza tena kuelekea mwishoni mwa mwaka jana ambapo alilazimika kuiacha timu mikononi mwa kocha msaidizi Jordi Roura ambaye alichukua nafasi yake.
Villanova alirejea mwezi Januari na safari hii amelazimika kuachia ngazi kwa muda mrefu ili atibiwe .
0 Maoni/comments: