HICHI NDO ALICHOKISEMA NANDO BAADA YA KUTOLEWA KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER
Posted in Nando
Nando akiwa na Dj Fetty wa Clouds FM
|
Nando ambaye aliondolewa wiki iliyopita kwa kuvunja miongoni mwa sheria za shindano hilo alikuwa akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“I live my life with no regrets,”alisema Nando.
“Sitaki sijui matatizo wala nini, kilichotokea ndio kimetokea, najipanga upya naendelea na maisha mengine. Vingapi vimetokea vingine vizuri nyuma mpaka unapoenda vinakuja vizuri na vizuri kila siku? Tokea nilipotokea mimi nilipokuwa mtoto mdogo nani alikuwa ananijua? Sasa hivi nipo peace yaani, nashukuru kwamba mmenipokea vizuri. Naendelea na maisha, uzuri nimepata platform ya kutengezeza jina langu, kwahiyo naenda hivyo hivyo mpaka huko ntakapofika.”
0 Maoni/comments: