 |
Napenda kumshukuru Mungu kwa siku ya leo napenda kuwashukuru tigo na wasanii wengine walioudhuria na kufaanikisha Bash hii kiujumla kabisa..... Wasanii wote walipanda lakini kutokana na ratiba sisi tulikuwa wa mwisho kupanda jukwanii kuja kukonga nyoyo za mashabiki wangu na wateja wa tigo min kabang.....Sikuwa pekee yangu kwenye stage nilikuwa na dancers wangu wote kuhakikisha nakata kiu ya wana Mwanza na kuacha historia mbele ya maelfu waliofurika kwenye uwanja wa c.c.m kirumba.... na kuhakikisha kuwa Min kabang ipo poa ... Sikuamini nilipotokea jukwanii ule umati wa maelfu ya watu wakubwa kwa wadogo waliofurika ndani ya uwanja huu na kikubwa kilichonisisimua ni shangwe za mashabiki baada tu ya mimi kutokea ni umati ulionikumbusha show ya leka dutigite mkoani kigoma umati uliokuwa umefurika kipindi kile ni sawa sawa na niliouona leo ccm kirumba..kiukweli watu wa mwanza wameonyesha mapenzi ya hali ya juu kiasi ilibidi show kusitishwa baada ya purukushani zilizotokea nikiwa ndiyo kwanza nimeimba wimbo mmoja tu wa nimpende nani..ile hali ya mkanganyiko wa watu kusukumana ilisababisha binafsi kuacha kuimba kutokana kuona maelfu ya mashabiki kuumizana na kukanyagana kutokana msongamano wa watu..... Nasikitika kwa hali iliyotokea uwanjani pale mashabiki waliokuwa wakisubiri kwa hamu kushuhudia show yangu nzima ikiishia njiani, narudi Dar lakini nawaahidi mashabiki zangu wa mwanza kuwa i will be back..nawaandalia kitu kikubwa na kizuri hapo hapo CCM KIRUMBA panapomajaliwa tuombeane uzima kuja kuona kile walichokuwa wanakitegemea leo na maujuzi mengine zaidi yatakayokuwa yameongezwa.... Zifuatazo ni picha kadhaa nikijimwaya mwaya stejini na silaha zangu hatari kabisa Emma Platnum,Moses Iyobo,Dumi Utamu & Rama Mpauka kufanya maangamizi haya kwenye Music on Sound My Blood Rommy Jones kuhakikisha sound na mic zikienda sawa....!! |

|
0 Maoni/comments: