Jun
2013
14
KOMBE LA MABARA 2013 | CONFEDERATIONS CUP 2013 NCHINI BRAZILI KUANZA KESHO
Posted in Brazil, FIFA Confederations Cup, Fifa World Cup 2014, Japan, World Cup 2014 BrazilIFUATAYO NI TATHMINI YA MECHI HII YA UFUNGUZI!
Hali za Wachezaji
Brazil wanatarajiwa kutumia Mfumo wa 4-2-3-1 huku Staa wao Neymar akicheza nyuma ya Straika Fred na langoni kuwepo Kipa Julio Cesar ingawa Kocha Luiz Felipe Scolari atalazimika kuamua nani aanze Fulbeki ya kushoto kati ya Marcelo au Filipe Luis.
Japan wanaweza kumkosa Mchezeshaji wao mkubwa Keisuke Honda na hilo linaweza kumfanya Shinji Kagawa akacheza kama Kiungo wa kati badala ya Kiungo wa pembeni kama anavyochezeshwa akiwa na Japan.
Nahodha wa Japan Makoto Hasebe atarudi tena dimbani baada ya kutumikia Kifungo cha Mechi moja.
Tathmini ya Mechi
Hiki ndio ‘Kipima Joto’ rasmi kwa Brazil kuweza kuwa Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia Mwakani na pia kama wataweza tena kurudia utawala wao wa Kombe la Dunia kwani wao ndio Nchi iliyotwaa Kombe hilo mara nyingi walipolichukua mara 5.
Brazil, kama Wenyeji wapo Fainali hizo za Kombe la Dunia, na Wiki iliyopita Japan ilikuwa Nchi ya kwanza Duniani kuungana nao kwenye Fainali hizo baada ya kufuzu kutoka Kanda ya Bara la Asia.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
GLT==TEKNOLOJIA YA MSTARINI GOLINI KUTUMIKA:
-FIFA imethibitisha, GLT, Goal Line Technology, kuamua kama Mpira umevuka Mstari wa Golini na hivyo ni Goli halali, itaanza kutumika rasmi kwenye Mashindano rasmi kwenye Kombe la Mabara kuanzia Mechi ya Ufunguzi kati ya Wenyeji Brazil na Japan.
-GLT itakuwepo Viwanja vyote 6 huko Brazil vitakavyotumika kwa Mechi za Kombe la Mabara
-FIFA imesisitiza GLT ni msaada tu kwa Marefa na Marefa hao ndio wanabaki Waamuzi wa mwisho kama ni Goli au si Goli.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
Kwa Brazil hii ni Mechi ya kwanza ya Mashindano rasmi yanayotambuliwa na FIFA baada ya Miezi 23, tangu walipotolewa Robo Fainali ya Copa America na Paraguay Mwaka 2011 na hilo limewafanya waporomoke kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani na kushika Nafasi ya 22.
Brazil wanatinga Mechi hii wakiwa wameshinda Mechi 2 tu kati ya 9 walizocheza mwisho lakini sasa wapo chini ya Kocha mzoefu Luiz Felipe Scolari ambae alishika mikoba Novemba Mwaka jana.
Japan hawajawahi kuifunga Brazil katika Mechi 9 walizocheza nao ambazo wamefungwa 7 lakini Kikosi cha sasa, maarufu kama Blue Samurai, chini ya Kocha toka Italy, Alberto Zaccheroni, ni bora katika Historia yao kikiwa na Vipaji kama vile Kiungo wa Manchester United Shinji Kagawa.
Chini ya Kocha Alberto Zaccheroni, Japan imeshawahi kuifunga Argentina inayoongozwa na Lionel Messi na pia kuifunga France Mwezi Oktoba Mechi iliyochezwa Nchini France.
Zaccheroni ametamba: "Huko Ulaya, ninakotoka, Watu wengi wanafikiria Dunia haibadiliki! Mie sifikirii hivyo!"
Uso kwa Uso
-Brazil wameifunga Japan mara 7 na Sare 2 huku wakifunga Jumla ya Bao 24-4.
-Sare 2 ni za Kombe la Mabara za 0-0 Mwaka 2001 na 2-2 hapo 2005
-Mara ya mwisho kukutana katika Mechi ya Kirafiki Oktoba Mwaka Jana Nchini Poland, Brazil iliinyuka Japan 4-0 na Neymar, kufunga Bao 2, na nyingine ni za Paulinho na Kaka
Dondoo Muhimu
Brazil
-Brazil ndio Timu yenye mafanikio makubwa kwenye Kombe la Mabara kwa kulitwaa Miaka ya 2009, 2005 & 1997.
-Wakitwaa Mwaka huu, Brazil watakuwa Nchi ya kwanza kulichukua mara 3 mfululizo.
-Kwenye Kikosi cha sasa cha Brazil, Wachezaji pekee waliobakia ambao walicheza Kombe la Mabara lililopita la Mwaka 2009 ni Kipa Julio Cesar na Dani Alves.
-Fred ameifungia Brazil Bao 5 katika Mechi zao 6 zilizopita.
Japan
-Japan, mara pekee waliyofanya vyema kwenye Kombe la Mabara, ni Mwaka 2001walipomaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa France lakini mara zote zilizobakia hawajavuka hatua ya Makundi.
-Japan wameshinda Mechi 1 tu kati ya 4 walizocheza mwisho na kabla ya hapo walishinda 6 kati ya 7.
-Shinji Okazaki amepiga Bao 5 kati ya Mechi 6 Japan walizocheza mwisho.
VIKOSI VINATARAJIWA:
BRAZIL [Mfumo 4-2-3-1]:
Julio Cesar
Alves, David Luiz, Thiago Silva, Marcelo
Paulinho, Luiz Gustavo
Hulk, Oscar, Neymar
Fred
JAPAN [Mfumo 4-2-3-1]:
Kawashima
Uchida, Yoshida, Konno, Nagatomo
Endo, Hasebe
Okazaki, Honda, Kagawa
Maeda
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KOMBE LA MABARA
MFUMO & RATIBA:
MAKUNDI:
KUNDI A:
-Brazil
-Japan
-Mexico
-Italy
KUNDI B:
-Spain
-Uruguay
-Tahiti
-Nigeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
VIWANJA:
-Estadio Mineirao - Belo Horizonte
-Estadio Nacional de Brasilia - Brasilia
-Estadio Castelao - Fortaleza
-Arena Pernambuco - Recife
-Estadio Do Maracana - Rio de Janeiro
-Arena Fonte Nova - Salvador
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
JUNI 15
Saa 4 Usiku
Brazil v Japan [Brasilia]
JUNI16
Saa 4 Usiku
Mexico v Italy [Rio De Janeiro]
Saa 7 Usiku
Spain v Uruguay [Recife]
JUNI 17
Saa 4 Usiku
Tahiti v Nigeria [Belo Horizonte]
JUNI 19
Saa 4 Usiku
Brazil v Mexico [Fortaleza]
Saa 7 Usiku
Italy v Japan [Recife]
JUNI 20
Saa 4 Usiku
Spain v Tahiti [Rio De Janeiro]
Saa 7 Usiku
Nigeria v Uruguay [Salvador]
JUNI 22
Saa 4 Usiku
Japan v Mexico [Belo Horizonte]
Italy v Brazil [Salvador]
JUNI 23
Saa 4 Usiku
Nigeria v Spain [Fortaleza]
Uruguay Tahiti [Recife]
NUSU FAINALI
-JUNI 26
[Belo Horizonte]
[SAA 4 USIKU]
Mshindi A v Mshindi wa Pili B
JUNI 27
[Fortaleza]
[SAA 4 USIKU]
Mshindi B v Mshindi wa Pili A
MSHINDI WA TATU
-JUNI 30
[Salvador]
[SAA 1 USIKU]
FAINALI
JUNI 30
[Rio De Janeiro]
[SAA 7 USIKU]
0 Maoni/comments: