Sunday, May 5, 2013

0

ISINGEKUWA LADY JAY DEE, NINGEMUOA VANESSA MDEE - GADNA G. HABASH

Posted in , ,

Mume wa Legend wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jadee’, Gardner G Habash ‘Kapteini’ aliwaacha watu midomo wazi baada ya kusema kama angekuwa hajaoa, basi angemuoa msanii anayekuja kwa kasi kwenye gemu, Vanessa Mdee.

Kapteini alitamka hayo juzi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Dar Indian Ocean 2013 kilichochukua nafasi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mume huyo wa Lady Jaydee alikuwa MC wa shughuli hiyo hivyo kutumia kipaza sauti kumnadi Vanesa.
“Kiukweli Vanessa ni msanii mzuri, ana uwezo mkubwa wa kufanya muziki wa Hip Hop na kulitawala jukwaa. Ningekuwa sijaoa kwa kweli ningemuoa Vanesa Mdee,” alisema Gardner.
Mbali na Vanessa, wasanii wengine wanaounda familia ya B-Heatz walipata nafasi ya kutumbuiza katika hafla hiyo.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ