ZITTO NA DIAMOND WAIPONDA SERIKALI WAZI
Posted in Diamond Platnumz, Zitto KabweZitto Kabwe na Diamond wameamua kuzungumza kila wanachoona sio sawa na kinachofanywa na serikali yetu huku wote wakionyesha uchungu walionao kutetea maslahi ya jamii inayowazunguka, kupitia ukurasa wake wa facebook, hiki ndicho alichokiandika Mbunge Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe
Serikali
inasema kampuni za simu zinalipa kodi nyingi. Kodi gani? VAT! Nani
kasema VAT inalipwa na kampuni? Hii Ni kodi ya walaji kama ilivyo ushuru
wa bidhaa (excise duty). Serikali inasema kampuni za simu hazilipi kodi
ya mapato Kwa kuwa zimewekeza sana, tshs 2.5 trilion! Nani kakagua huo
uwekezaji? Eti Kwa miaka 5 kodi ya makampuni iliyolipwa Ni tshs 64bn,
wastani wa tshs 12bn Kwa mwaka. Rwanda yenye idadi ya watu sawa na
wateja wa Vodacom peke yake mwaka 2010 walikusanya corporate tax $14m,
Tanzania ilikusanya $1.4m tu. Serikali iache blah blah, ikusanye kodi.
TCRA ipewe Nguvu ya kukagua uwekezaji wa makampuni kama ilivyo TMAA
kwenye madini. Inatosha sasa
Wakati huohuo Diamond nae alionyesha machungu aliyonayo kwa serikali kwa
kushindwa kutambua mchango wao na kudai wanatumiwa wakati wa kampeni za
viongozi lakini baada ya kufanikiwa na walichukuwa wakikitaka
wanawasahau wasanii..
hiki ndicho alichokiandika kupitia instagram
"Dah!
hivi kweli Serikali imekosa majibu ya swali la mh: Mbunge kuhusu mapato
ya biashara ya ringtones..!? Kweli sasa naanza kuamini kuwa Serikali
Inatukumbatiaga tu kwa Mda mfupi na kututumia Wasanii kwenye Kampeni zao
kwa Maslahi yao Binafsi, kisha wanatu Damp Baada ya kufanikiwa kwenye
Uchaguzi wao, bila kujali Thamani na Mchango wetu kwao...."
0 Maoni/comments: