BAADA YA KUWASANUKIA CLOUDS TWITTER, JAY DEE AZINGUANA TENA NA BEN POL.
Posted in Ben Pol, Lady Jay Dee
So much is happening on Twitter these days. Wengi mnafahamu anachokiandika Lady Jaydee siku za hivi karibuni na sasa kibao kimemuendea Linah na Ben Pol.
Lady Jaydee anadai wasanii wa THT wamemsaliti kwa kile anachodai walikatazwa kwenda kuperform Nyumbani Lounge licha ya kuwalipa advance.
“Linah na Ben Pol mnabisha hamkukatazwa? Nisalitini ila hamtapata faida mtatoka kapa pia,” ametweet Jide.
Shutuma hizo zimepolekewa kwa hasira na Ben Pol aliyemjibu Jaydee:
“Hiyo show kulikuwa na wengine pia wakuperform je wali perform? kama nililipwa nanikashindwa ku show up, mbona sidaiwi?? Tafakari.”
Aliongeza, “Ben Pol hana muda wa maneno na majungu. Ombi langu ni mmoja kwako. Put me out of your business. PERIOD.”
“Don’t talk about things you don’t know about. DON’T.”
“Ukiwaza kutumia akili kamwe huwezi kukosea, ila utakapotumia hisia lazima ujikanyage somewhere. Nimekua vya kutosha #Trustme,” alimalizia Ben.
Unazungumziaje hiki kinachooendelea sasa na athari yake kwenye muziki wa Tanzania. Maoni yako tafadhari.
0 Maoni/comments: