Wednesday, December 12, 2012

0

UJUMBE WA KWANZA WA PAPA BENEDICT, TOKA AFUNGUE AKAUNTI YA TWITTER

Posted in
Papa Benedict wa 16 ametuma ujumbe wake wa kwanza kwenye akaunti yake yaTwitter. Ujumbe huu ulikuwa umesubiriwa kwa hamu sana.
Alionekana akibonyeza kwenye tabiti yake ya iPad na kutuma ujumbe huo.
Ujumbe wake ulikuwa unasoma hivi '' Marafiki wapendwa, nimefurahi sana kuwasiliana nanyi kupitia Twitter. Asanteni sana kwa ujumbe wenu na ninawabariki nyote.''
Msemaji wake alisema kuwa ujumbe wa Papa utafikia kila mtu amjuaye kwa kutumia akaunti zake zilizo kwenye lugha saba.
Akaunti ya papa iliyo kwenye lugha ya kiingereza tayari ina wafuasi zaidi ya laki sita.
Akaunti zake zote ambazo ni @pontifex zinafuatana moja baada ya nyingine.
Mwaka jana Papa alituma ujumbe wake wa kwanza kutoka Vatican kuweza kuzindua mtandao wake wa maelezo mbali mbali.
Papa ni kiongozi wa waumuni bilioni 1.2 wa kikatoliki na atakuwa akitia saini ujumbe wake wala hatoundika mwenyewe.

Ujumbe wa papa kupitia Twitter unatarajiwa kuwajibu wafuasi wake kila wiki , kutoa baraka za Jumapili pamoja na kauli yake kuhusu matukio duniani.

Akaunti ya twitter ya Papa Benedict
Vatican imekuwa ikijaribu kutumia teknolojia za kisasa za mawasiliano kueneza imani, huku mwasisi wa Redio,
Guglielmo Marconi, akizindua redio ya kwanza ya Vatican mwaka 1931.
Kanisa Katoliki, pia tayari linatumia mitandao kadhaa ya kijamii ikiwemo ujumbe mfupi na YouTube, kuwasiliana na vijana.
Wasaidizi wa Papa wanasema kuwa papa mwenyewe, bado anapenda kuwasiliana na watu kwa maandishi kuliko kutumia komputa.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ