MWANADADA KEISHA KU-SHOOT VIDEO YA NYIMBO YAKE ''NIMECHOKA'' ALIYOPIGA NA DIAMOND
Posted in Diamond Platnumz, Keisha
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Keisha, amesema kuwa baada ya kuachia audio ya ngoma yake mpya ya ‘Nimechoka’ aliyopiga na Diamond sasa yupo mbioni kupiga video ya wimbo huo kwa lengo la kuonesha uhalisia wa mambo juu ya kazi hiyo.
Ngoma hii inahusu maisha halisi ya mapenzi kwa mwanamke ambaye mara zote anakuwa na upendo wa dhati lakini mwanaume haoneshi na anajali upendo huo ndipo mwanamke anapoamua kusema ‘Nimechoka’.
Keisha ambaye aliwahi kutamba na ngoma zake kama ‘Usinicheke’ kazi iliyokuwa inazungumzia ulemavu wa ngozi, ‘Uvumilivu’, ‘Nalia’ na nyingine kibao zilizoweza kumweka katika nafasi nzuri kimuziki.
Keisha alizungumza na DarTalk na kusema kuwa ujio wake huo ni mzuri kwani tayari ngoma yake hiyo inafanya vizuri, hivyo anaamini mashabiki wake watapenda kuona uhalisia kutoka kwenye video.
“Sipo kimya sana kwa sababu tayari nimeshafanya ngoma na ‘Diamond’ na sasa natarajia kuanza kupiga picha ya video pale kwa Adam Juma hivyo mashabiki wangu wakae tayari kusubiri video hiyo,” alisema.
Aliongeza kuwa mara nyingi anakuwa kimya kutokana na mambo fulani fulani, ikiwemo mtoto wake kwani hataki kumuacha muda mrefu akiwa na msichana wa kazi.
Mtoto wa Keisha |
0 Maoni/comments: