Awilo Longomba ni
mwanamuziki wa
Kongo ambaye alikuwa mpiga ngoma katika bendi za
Viva la Musica,
Stukas,
Nouvelle Generation na
Loketo. Mwaka wa
1995, hatimaye aliacha kupiga ngoma na kuamua kuimba na alitoa albamu yake ya kwanza, Moto Pamba, baada ya kupata msaada kutoka
Shimita,
Ballou Canta,
Dindo Yogo,
Dally Kimoko,
Sam Mangwana,
Syran Mbenza na
Rigo Star.

CD yake ya pili,
Coupe Bibamba (mwaka wa
1998) ilimfanya ajulikana kote barani Afrika, Ulaya na Amerika. Hii ilifuatiwa na
Kafou Kafou (mwaka wa
2001) na albamu yake ya hivi karibuni,
Mondongo (mwaka wa
2004), ambayo inawashirikisha
Japponais, Dally Kimoko,
Caen Madoka,
Djudjuchet,
Josky na
Simaro Lutumba. Pia alishirikishwa kama atalaku (mtu wa kutumbuiza) katika baadhi ya rekodi za
soukous.
Awilo kwa sasa anaishi nchini
Ufaransa na ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Barbara Kanam.
Jamaa ya Awilo katika sekta ya muziki ni pamoja na baba yake Victor Longomba mwanac
hama mwanzilishi wa
TP OK Jazz na vilevile Longombas ambalo ni kundi maarufu la afro
-fusion lenye makao nchini
Kenya.

Mnamo mwaka wa
2008 Awilo Longomba alitoa albamu mpya, SUPER
-MAN,
ambayo ilikuwa fanikio nyingine kubwa. Awilo aliendelea na umaarufu
wake nchini Marekani / Kanada huku akiwa katika ziara pamoja na Nabtry
International Cultural Dancers (kundi la kitamaduni la kimataifa la
kusakata au kucheza ngoma) kundi ya Kiafrika ya kucheza ngoma
iliyoanzishwa mwaka wa 2007 na Grace Haukwa. Ziara ya SUPER
-MAN
ilikuwa yenye mafanikio makuu miaka za 2008 na 2009. Kutokana na kura
za umaarufu na ushindi wa kihistoria katika Tuzo za Reggae ya Kimataifa
na Muziki wa ulimwengu huku nchi zaidi ya 120 zikipiga kura, albamu mpya
ya Awilo, SUPER
-MAN,
ilishinda TUZO LA MTUMBUIZAJI BORA WA SOUKOUS WA MWAKA WA 2009.
Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Nabtry GRACE HAUKWA ambaye
anamwakilisha Awilo nchini
USA alikuwepo kupokea tuzo hilo kwa niaba ya Awilo katika sherehe ya Tuzo za Reggae ya Kimataifa na Muziki wa ulimwengu.
Source:
Awilo Longomba Wikipedia
0 Maoni/comments: