Monday, September 3, 2012

0

Stoke City Yamng'ang'ania M.Owen, Huku Meireles Kuihama Chelsea Kwenda Fenerbahce

Posted in ,
Stoke City yategemea kumsaini Michael Owen
Meneja wa Stoke City Tony Pulis amebainisha kuwa wapo mbioni kumsaini aliekuwa Straika wa Manchester United Michael Owen kwa Makataba wa ‘cheza ulipwe.’
Pulis amesema wana nia thabiti ya kumchukua Michael Owen, Miaka 32, ili awasaidie na amesema watampa Mkataba kama ule wa Difenda Jonathan Woodgate ambae hulipwa tu akicheza kwa vile Mchezaji huyo, kama Owen, huandamwa mara kwa mara na majeruhi.
Kwa vile Michael Owen ni Mchezaji ‘Huru’, baada ya kuachwa na Manchester United, anaruhusiwa kusaini na Klabu yeyote licha ya Dirisha la Uhamisho kufungwa juzi Ijumaa Agosti 31 hadi Januari Mwakani na mwanya huo sasa umemfanya Owen awe lulu kwa Klabu nyingi, hasa Liverpool na Sunderland, ambazo zinasemekana pia zinamwania.


Raul Meireles kuihama Chelsea kwenda Fenerbahce
Klabu ya Uturuki Fenerbahce imetamka kuwa Mchezaji wa Chelsea ambae pia ni Kiungo wa Kimataifa wa Portugal Raul Meireles yupo kwao akipimwa afya kabla hajakamilisha Uhamisho.
Fenerbahce wanaruhusiwa kumnunua Kiungo huyo mwenye umri wa Miaka 29 kwa vile kwao Dirisha la Uhamisho linafungwa kesho kutwa Jumatano.
Meireles alijiunga na Chelsea Mwaka mmoja uliopita akitokea Liverpool.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ