IRENE UWOYA NA HALLE BERRY KUIGIZA PAMOJA??
Posted in Halle Berry, Irene UwoyaHalle Berry ni moja ya wasanii mahiri kabisa ambao wana uwezo mkubwa kwani ameweza kuonesha uwezo wake kwenye filamu kama ‘Die Another Day’, Catwoman, New Year’s Eve, Monster’s Ball na nyingine nyingi.
Ishu ya Uwoya kushiriki ndani ya filamu moja na mwanadada huyo inadaiwa kuwa katika mazungumzo anayofanya nchini Uingereza mmoja ya wadau wakubwa ya tasnia hiyo kutoka Marekani ndiye aliyempa ishu hiyo baada ya kuona baadhi ya filamu alizocheza pamoja kujiamini kwake.
Uwoya alidai kuwa bado hajaamini kwani hajapewa ishu kamili na ameambiwa kuwa atajulishwa kwa njia ya email endapo kila kitu kitakuwa sawa kwa sababu ya ratiba ya Berry.
“Naweza kucheza filamu moja na Halle Berry, ingawa sijajua kama ishu hii inaweza kuwa kweli kwa sababu kama unavyojua kila kitu huwa kinaenda kwa ratiba siyo kama sisi bongo filamu tunajitolea bila hata kufuata ratiba,” alidai.
0 Maoni/comments: