Bifu La John Teery na Anton Ferdinand Kuendelea Jumamosi??
Posted in Anton Ferdinand, Chelsea, John Terry, QPR
>>KUCHEZWA Septemba 15, SWALI Wachezaji watapeana mikono??
Ipo minong’ono John
Terry hatapewa mkono na Anton Ferdinand wakati Timu hizi zitakapokutana
Jumamosi Septemba 15 katika Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Loftus
Road.
Hadi sasa Ligi Kuu haijatoa tamko kama
itazuia ile desturi ya Timu kupeana mikono kabla ya Mechi kama
ilivyofanya mara ya mwisho Timu hizi kukutana Mwezi Aprili ili kuepusha
shari kati ya Nahodha wa Chelsea John Terry na Beki wa QPR Antoin
Ferdinand ambao walikwaruzana kwenye Mechi Uwanja wa Loftus Road Mwezi
Oktoba Mwaka jana na hatimae Terry akafikishwa Mahakamani na kushitakiwa
kwa kukashifu kibaguzi lakini akashinda Kesi hiyo.
Wakati FA ikiwa bado haijatoa hukumu
yake dhidi ya Terry, inasadikika bado ipo mikwaruzo kati ya Wachezaji
hao na ndio maana Wadau wanaifuatilia sana Mechi ya QPR na Chelsea
Jumamosi ijayo.
Mwishoni mwa Mwezi huu, Terry
anatarajiwa kwenda mbele ya Jopo maalum la Chama cha Soka England, FA,
ili kujitetea binafsi katika Kesi hiyo yake inayomuhusu Ferdinand baada
ya yeye mwenyewe kuomba kufika mwenyewe mbele ya Jopo la FA ili kutoa
utetezi wake.
Baada ya tukio kwenye Mechi hiyo ya
Oktoba Mwaka jana, QPR na Chelsea zimeshakutana mara mbili, Mwezi
Januari kwenye FA Cup na Aprili kwenye Ligi, na mara zote hizo kupeana
mikono kabla ya Mechi kulifutwa ili kusichochee ugomvi zaidi.
Safari hii, Ligi Kuu inasemekana itafuta utaratibu wa kupeana mikono ikiwa tu itaombwa na moja ya Klabu hizo mbili.
CHANZO: Soka In Bongo
CHANZO: Soka In Bongo
0 Maoni/comments: