SERENA & VENUS to cross the Atlantic Ocean with two titles.
Ilikuwa ni siku ya aina yake ndani ya Wimbledon Tennis Park,eneo lilojaza viwanja au court 20 za tennis huko Kusini-Magharibi mwa London.
Bingwa mara nne Serena Williams akikutana na msichana anayechipukia na anayecheza fainali yake ya kwanza Agniezska Radwanska raia wa Poland.Msichana huyo mdogo mwenye matatizo na mfumo wake wa kupumua(respiratory system) alionyesha wazi anapoteza hii game baada ya kunyukwa vya kutosha set ya kwanza 6-1,lakini alionyesha ujasiri na kuthibitisha kuwa aliingia fainali kwa malengo baada ya kurudisha kibano na kumzuia Serena kushinda mapema kwa kumchapa 7-5 katika set ya pili.Set ya tau,decider set ndo ilikuwa na mshikemshike baada ya Radwanska kushinda subset 2-1 za mwanzo kabla ya Serena kurudi na kumchapa aces 4 mfululizo na kufanya iwe 2-2.Baada ya hapo kilichofuatia ni kipigo mteremko hadi Mmarekani Serena alivyotangaza ubingwa kwa 6-2 na kufanya jumla ya matokeo kusomeka 6-1,5-7 na 6-2.
Ushindi huu ni wa kwanza kwa Serrena aliyekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu na wakati mwingine kuhitaji kulazwa hata hospitali baada ya kusumbuliwa na tatizo la blood clotting!!
Mara ya mwisho anashinda ilikuwa ni mwaka 2010 na kwa sasa kashajikusanyia 14 grand slams kwa ujumla katika Wimbledon pekee.!
+
Katika tukio la kushangaza,Serena baada ya kushinda aliruka na kwenda kukimbilia walipokuwa wameketi baba,dada,mama na ndugu zake wa karibu na kwenda kuwakumbatia.Ikumbukwe kuwa baba yake mzazi ndio kocha wake na ndio aliyemuingiza kwenye ulimwengu wa Tennis.
Baadae Serena alitoa hotuba fupi ya shukrani huku machozi yakimlenga kwa kuelezea aliyoyapitia hospitalini na hadi kufikia hatua ya kudhani hatorudi tena uwanjani.
Katika tukio lingine Serena alijiunga na dada yake katika fainali nyingine hapo usiku na kufanikiwa kunyakua taji la Wimbledon Women's Double.
Serena aliamua kusitisha sherehe za ubingwa wake kwa muda na kuingia uwanjani kukipiga wakiwa na dada yake mkubwa Venus Williams,wapinzani wao walikua ni raia wa Czech Andrea Hlavackova na Lucie Hradecka.Iliwachukua dakika 38 kuandikisha ushindi wa 7-5,6-4 uliochangiwa kwa kiasi kikubwa na dada mkubwa Venus aliyekuwa akipiga aces za kutosha.
Ikumbukwe pia ndugu hawa hawajawahi kupoteza kwenye fainali ya pamoja.Na sasa wapenzi na mashabiki wao wanawasubiri kwa hamu hapo mwishoni mwa mwezi huu kwenye Olympics zinazofanyikia London tena.
All the best the Williams!
.

0 Maoni/comments: