Hussein Machozi afanya ngoma na mwanadada Size 8 wa Kenya
Posted in Hussein Machozi, Size 8Mwanamuziki wa Tanzania Hussein Machozi amefanya ngoma na msanii wa kike Size 8 anayetemba sana kwa sasa nchini Kenya pamoja na Afrika Mashariki.
Wimbo huo ambao umefanyika katika studio za Ogopa Djs za nchini humo unaitwa Addicted.
Machozi anasema wimbo huo ni kwaajili ya mashabiki wake wa kike ambapo video ya wimbo huo itafanywa na kampuni ya Ogopa DJs.
Kwa sasa Size 8 ambaye jina lake halisi ni Linet Masiro Munyali anakimbiza na club banger yake iitwayo Vidonge.
Mwaka jana msanii huyo alitajwa kuwania tuzo za Chagua La Teeniez za Kenya kwenye kipengele cha mwanamuziki bora wa kike.
Hii si mara ya kwanza kwa Hussein Machozi kumshirikisha msanii wa Kenya kwani tayari ana wimbo alioufanya na mwanadada Habida uitwao Asante.
Source: bongo5.com
0 Maoni/comments: