Saturday, November 6, 2010

0

Phiri: Mimi ni wenu tu na nitabaki kuwa wenu

Posted in
Imeamua kumuongezea mkataba huku ikimpandisha cheo hadi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi kocha wao, Mzambia Patrick Phiri.




Hiyo si nyingine bali ni ile kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba, ilisema uamuzi wa huo wa kamati ya utendaji ni sehemu ya jitihada za kuiendesha kisasa zaidi na kufuta hofu iliyoanza kuwepo kwa baadhi ya mashabiki kwamba kocha huyo ataiama klabu yao mara baada ya mkataba wake hapo Novemba 9 mwaka huu.

Kamati hiyo pia imeunda Kamati ya Ufundi yenye wajumbe nane na kumrejesha klabuni hapo mchezaji na kocha wa zamani wa ‘Wekundu wa Msimbazi’, Abdallah Kibadeni, atakayekuwa kocha wa timu yao ya vijana.

Akilonga jana na wana darhotwire, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alisema maamuzi hayo kuhusu Phiri yametolewa katika kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika juzi.

Alisema vilevile kuwa lengo la kumuongezea mkataba Phiri na kumpa jukumu jipya la kuwa Mkurugenzi wa Ufundi ni kujiweka sawa kwa maandalizi ya michuano ya kimataifa ambapo Simba itaiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.

"Kamati ya Utendaji ya Simba imempandisha cheo mwalimu Patrick Phiri kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu kuanzia Novemba 3 mwaka huu," alisema Rage.

Alisema vilevile kuwa kamati hiyo iliamua kuunda kamati ya ufundi ya watu nane kwa lengo la kuboresha vikosi vya timu zao za vijana.

Rage aliwataja wajumbe hao kuwa ni Kibaden, Ibrahim Masudi (atakayekuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo), Said Tully, Khalid Abeid, Arthur Mambeta, Patrick Phiri, Dan Manembe na Katibu Mtendaji, Evodius Mtawala, ambaye ndiye atakayekuwa katibu wa kamati hiyo.

Phiri hakupatikana jana kuzungumzia msimamo wake baada ya Simba kutangaza uamuzi wa kumpandisha cheo na pia kumuongezea mkataba wa kuifundisha klabu yao.

Mkataba wa Phiri unadaiwa kuwa utamalizika Novemba 9 na kulikuwa na taarifa zinazodai kuwa atatimkia klabu ya Azam ambayo hivi sasa haina kocha baada ya kusitisha mkataba wake na Mbrazil Itamar Amorin.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ