Next
Previous
Showing posts with label Agness Masogange. Show all posts

Wednesday, August 21, 2013

0

ALICHOKISEMA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUHUSISHWA NA MADAWA YA KULEVYA

Posted in , , ,
  


MSANII Wa Muziki wa Bongofleva mwenye jina kubwa Town na mwenye Mkwanja mkubwa hapa nchini Nasseeb Abdulmaliki “Diamond Platnumz” amejitokeza na kukanusha kuwa hahusiki na biashara ya madawa ya kulevya.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa za Diamond kujihusisha na biashara hiyo hasa kutokana na ukaribu wake na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini.

 Taarifa zaidi zinasema ni wafanyabiashara hao waliohusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kifo chake ziligubikwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akikanusha taarifa hizo Diamond amesema  :

“Ni kweli mimi nina pesa za kutosha kuniwezesha kuishi maisha ninayotaka lakini sijawahi kujihusisha na biashara hiyo....

"Kufanya kazi kwa bidii kunalipa na kazi yangu inaonekana na ndiyo inayoniwezesha kuwa na fedha ambazo leo watu wameanza kuzitilia shaka. Sielewi nia ya watu hawa ni nini?”

Taarifa za Diamond kuhusishwa na mtandao huu zimeanza kushika kasi kufuatia miongoni mwa watu wake wa karibu kuonekana wakiwa karibu sana na akina Agnes Gerald “Masogange” (25) na Melisa Edward (24) kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere wa Dar es Salaam kabla hawajapanda ndege kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa.
0

TAARIFA JUU HABARI YA DIAMOND PLATNUMZ KUJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA

Posted in , ,
Kutoka Jamii Forums

Mwanamuziki Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond
*Utajiri, safari zake nje ya nchi vyatiliwa shaka
*Ahusishwa na mtandao hatari wa Masogange
KWA mara ya kwanza tangu lilipoibuka sakata la watu maarufu kujihusisha ama na utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jina la mwanamuziki anayeaminika kuwa na ukwasi mkubwa kwa sasa hapa nchini, Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond, limeanza kutajwa kuwa ni miongoni mwa vigogo wa ‘unga.’

Tayari mjadala mkubwa wa chini chini umeibuka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake, na taarifa ambazo zimelifikia MTANZANIA Jumatano kutoka vyanzo mbalimbali zimedai kuwa, mwenendo wa maisha ya Diamond sasa unachunguzwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.

Kutajwa kwa jina la Diamond katika sakata hili, kunatiwa nguvu zaidi na mwenendo binafsi wa maisha wa msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya, unaokwenda sambamba na ukwasi mkubwa alioupata katika kipindi kifupi.

Monday, August 12, 2013

0

KUHUSIANA NA KUSACHIWA MADAWA YA KULEVYA: JE NA WASANII WA BONGO MO0VIE KUKUMBWA NA AIBU HIYO??

Posted in , ,
Wema Abraham Sepetu



Hamad Ali




KWELI Waswahili usema kua uyaone, awali nilifikiri mjini ni maghorofa kumbe ni zaidi ya hayo maghorofa, hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo fleva kupekuliwa Airport, wasanii wa muziki huu kwa sasa si marafiki wa viwanja vya Ndege swali linakuja je wasanii wa filamu nao watapata jeraha hilo?
Kufuatia kashifa ya uvushwaji wa madawa ya kulevya inayolisakama Taifa la Tanzania wasanii wa muziki wa Bongo fleva wamekuwa waathirika wakubwa katika viwanja vya Ndege kwani inapofikiwa wakati wa kupekuliwa wanapekuliwa kweli kweli hadi wengine wanakasirika na kuhisi kama wanadharirishwa kwa kufanyiwa hivyo.
Ambwene YesayaWabongofleva ambao moja kwa moja wameonja adha ya kuhisi wanaweza kuwa na Ngada katika mabegi yao ni pamoja na Ambwene Yesaya AY ambaye alikutana na mkasa huo akiwa uwanja wa ndege na kutumia muda mwingi katika kupekuliwa hadi pale waliporidhika na kuona hana hatia na kuruhusiwa kuendelea na safari yake baada ya kujiridhisha.

Naye Raisi wa Manzese Hamad Ali aka Madee alikutana na kimbembe pale alipotua nchini Afrika ya kusini akiwa sambamba na Mzimbabwe wao pekee ndio waliowekwa kiti moto kwa kupekuliwa zaidi ya saa moja kwa kuvuliwa hadi nguo za nyepesi za ndani na mabegi yao kwa kumwaga nguo zote na baadae kuombwa radhi kwa muda wao na kupekuliwa sana.
Sasa watu wanajiuliza kuwa je hali hiyo kwa upande wa wasanii wa Bongo Movie nao wanaweza kukutwa na adha hiyo ? ya kupekuliwa hadi kutumia zaidi ya muda mrefu hata kudharirishwa kwa kukaribia kuvuliwa kufuli, hakuna anayejua kuhusu hilo kwani wengi wanaamini kuwa inawezekana kwa sababu wanasafiri sana tofauti na waigizaji maswali ni mengi.

Pengine historia nayo inachangia hadi leo kwa wasanii wa filamu hakuna taarifa sahihi kuhusu kashifa ya matumizi ya madawa ya kulevya kwa waigizaji jambo ambalo limekuwa likiripotiwa kila siku kwa wasanii wa Bongo fleva pamoja na watu wao wa karibu kama wapenzi wao na Video queen ambao tayari wamekamatwa na madawa ya kulevya.

Sakata lilianzia pale Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania,

Sunday, August 11, 2013

0

HII NDO ATHARI YA KUWEKA PICHA ZA UCHI MTANDAONI

Posted in , ,


Mwezi wa kujistiri kwa wale wenzangu na mie ndiyo huo umeondoka, hapana shaka kuna wengine wanasoma hapa, huku wakiwa ndani ya yale mambo yetu. Siyo ishu, kila mtu ana uhuru wa kufanya kile akipendacho. Nchi yetu inaruhusu kuvaa chochote, ilimradi tu usiende utupu.

Nakumbuka miaka kama mitatu nyuma iliwahi kutokea hoja kuhusu mavazi, wengi walisema Serikali ilikuwa na mpango wa kupiga marufuku vimini na nguo za kubana.

Basi bwana siye tunaopenda mambo hayo roho zilikuwa juu, huku wengine tukitishia hata kuhama nchi ikiwa tutafikia huko kwa kukatazana mavazi.

Lakini kwa bahati nzuri rais wetu, Jakaya Kikwete alilitolea tamko suala hilo  na kusema kuwa kila mtu ana uhuru wa kuvaa kile anachojisikia, ili mradi tu asiende utupu. Hapo alimaliza kila kitu.

Tuachane na mambo ya mavazi, suala la msingi leo ni ‘mapicha’ na tattoo tunazochora mwilini na kuzitupia mtandaoni kila kukicha. Turudi kulekule kwenye uhuru wa kufanya kile unachojisikia, lakini usiku ukienda kulala jiulize mwisho wake nini?

Mimi na wewe hatujui kesho tutakuwa kina nani katika dunia hii, labda uniambie wewe huna ndoto za kufanya jambo litakalokufanya ukumbukwe, hata ukitoweka kwenye uso wa dunia.

Kila mtu, hasa wasichana waona fahari kuweka picha za nusu uchi  katika mitandao ya facebook, twitter na sasa instagram . Ujana, maji ya moto, kwa sasa hizo ‘likes’ na ‘comment’ unazopata zinakuvimbisha kichwa, lakini naamini baadhi yetu, miaka kumi ijayo tutatamani kurudi nyuma ili tuondoe historia mbaya tulioiweka mtandaoni.

Picha hizi zitatumika kukugandamiza kwa chochote unachokusudia kukufanya wakati huo. Ni nani atamchagua kiongozi mwenye picha kama zako unazotupia sasa.Kampuni gani yenye heshima itakayomwajiri mtu mwenye sifa mbaya kwa jamii.

Wednesday, August 7, 2013

0

HIZI NDO VIDEO MBILI ZA UCHAFU WA AGNESS MASOGANGE AMBAZO ZIMEPAGAWISHA WENGI

Posted in , ,


Tuesday, July 9, 2013

0

HUYU NDIYE ALIYEKAMATWA PAMOJA NA AGNESS HUKO SOUTH AFRIKA (KESI YA MADAWA)

Posted in ,
Inahisiwa kuwa  huyu mwanamke wa pili aliyetajwa na Kamanda Nzowa kwa jina la “Melisa Edward”  ni mdogo wake na Agnes ambaye katika akaunti ya facebook anayo tumia jina la (MELLIS EDWARD) , Agnes amemuweka katika orodha ya family kama ‘sister’ katika akaunti yake ya Facebook.




0

AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA

Posted in
HATIMAYE  wale Wanawake wawili walionaswa  na  madawa ya  kulevya  Afrika  kusini wametambuliwa kuwa  ni  mabinti  wa  KITANZANIA ..


Mabinti  hao  wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wetu  jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE)  ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita mtandao huu  ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Friday, May 3, 2013

0

HUYU NAYE ATAACHA LINI??: MWANADADA AGNESS MASOGANGE AENDELEA KUPIGA PICHA ZA MITEGO | ANGALIA HAPA

Posted in

Tuesday, October 9, 2012

0

SIWAFAGILII WANAUME WANAOSHOBOKA NA UMBO LANGU: AGNESS MASOGANGE

Posted in


Msanii wa Bongo movie  anayeuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva , Agness Gerald a.k.a Masogange amefunguka kuwa huwa hawafagilii wanaume au masharobaro wanaomshobokea  kwa sababu ya umbo lake linalodatisha wengi.

Akiongea na mwandishi wetu, mrembo huyo alifunguka kuwa mwanaume yeyote anayedai kudata na umbo lake ni mzushi na wala hana mapenzi ya dhati bali ni uroho wa ngono tu unaotokana na jinsi anavyoniona nilivyojaliwa.

“Mwanaume wa kweli anakupenda wewe mwenyewe jinsi ulivyo na si umbo lako ndiyo maana mimi siwafagilii kabisa wanaoshoboka kwa ajili ya umbo langu,”--Agness.
 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ