Jul
2013
12
NDONDI: TAARIFA JUU YA EVANDER KULETWA TANZANIA
Posted in Evander Holyfield, Francis Cheka, Mada Maugo, Ndondi
Jay Msangi ambae anaonekana katikati ameshawahi kucheza ngumi akiwa anaishi Marekani.
PromotaMtanzania Jay Msangi kutoka Hall of Fame Boxing and Promotions Company ameongea na Millard Ayo na kumwambia hiyo game imepangwa kuchezwa Uwanja wa Taifa April 27 2014 Uwanja wa Taifa ambapo Evander atapigana na Francois Botha wa South Africa aliewahi kuwa bingwa mara mbili.
Jay amesema haijawa ngumu kumpata Evander kwa ajili ya pambano kwa sababu kampuni yake ina uzoefu wa miaka mingi na imeshaandaa mapambano zaidi 30 kwenye jimbo la Ohio Marekani, ni kampuni ambayo iko Marekani na hapa Tanzania.
Hata hivyo kwa mara ya kwanza hii kampuni August 30 2013 itamkutanisha bondia Francis Cheka na Mmarekani Derrick atakaekua bondia wa kwanza Mmarekani kuja kupigana Tanzania.
Siku hiyohiyo ya August 30 pia mabondia Mada Maugo na Thomas Mashari watashuhudiwa wakizichapa live.
0 Maoni/comments: