NI CHELSEA VS MANCHESTER UNITED HAPO KESHO, LIVERPOOL NA EVERTON!!!
Posted in
Manchester United,
Shinji Kagawa,
Super Sunday

>>JUMAPILI DABI ya LIVERPOOL ya 219: Everton v Liverpool!
>>KAGAWA nje WIKI 4!!
>>JUA MAREFA wa KILA MECHI!!
Timu zote 20 za Ligi Kuu England
zitashuka dimbani kwa Mechi za Ligi Jumamosi na Jumapili kwa kucheza
Mechi 10 lakini kati ya hizo, bila shaka, BIGI MECHI itakuwa ile ya
Stamford Bridge ambayo vinara wa Ligi Chelsea wataivaa Manchester United
iliyo nafasi ya pili na Mechi ya mvuto ni ile DABI ya Jiji la Liverpool
Uwanjani Goodison Park kati ya Everton na Liverpool.
++++++++++++++++++++++
Lakini,
Manchester United watatinga huko Stamford Bridge huku wakiwa na habari
mbaya za kumkosa Kiungo wao mahiri kutoka Japan, Shinji Kagawa, ambae
atalazimika kuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 3 hadi 4 akiuguza goti aliloumia
kwenye Mechi na Braga iliyochezwa majuzi Jumanne.
Wakati, Sir Alex Ferguson anathibitisha
kukosekana kwa Kagawa pia alithibitisha kurudi tena Uwanjani kwa Chris
Smalling ambae alivunjika kidole cha mguu.
Msimu huu, Chelsea wamepoteza Pointi 2
tu kwenye Ligi na hawajafungwa hata Mechi moja na wako Pointi 4 mbele
ya Man United na wakiwa na Wachezaji hatari Eden Hazard, Juan Mata na
Oscar wamekuwa tishio katika mashambulizi yao.
Hilo linatambulika kwa Ferguson ambae
amesema: “Siku zote ni gemu ngumu kwa Chelsea na Man United. Unazo Timu
nzuri. Wote wapo juu baada ya kuanza vyema na Chelsea wanatumia mfumo wa
kuvutia na hilo lazima tulikabili. Wamewaleta Oscar na Hazard ni
Wachezaji wazuri. Wamemwingiza Mata ambae anafana uchezaji na kina Oscar
ambao wanacheza nyuma tu ya Straika wao mmoja. Si mfumo rahisi
kuukabili lakini lazima tutafute njia. Kwa sasa hawana Drogba tena na
wamebidi wabadilike. Walipokuwa na Drogba walikuwa wanaweza kucheza
mipira mirefu au kupitia kati. Sasa hayupo, ni moja kwa moja wanapitisha
mipira kupitia kati kwenye Kiungo.”
DABI: Everton v Liverpool
Tangu enzi hii ni mojawapo ya Dabi
inayoheshimika Duniani yenye ushindani mkali na hii ni Dabi ya 219
ambapo Liverpool wameshinda mara 87, Everton mara 66 na sare 65.
Katika Mechi 11 za Ligi Kuu ambazo Everton wamekutana na Liverpool wameshinda Mechi 1 tu, sare 3 na kufungwa 7.
Lakini, safari hii, Everton watajiona
kama wana nafasi kubwa kuifunga Liverpool hasa kwa vile wao wameanza
Msimu vizuri na wapo nafasi ya 4 kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa na Pointi
15 huku Liverpool wakiwa nafasi ya 12 na wana Pointi 9 tu.
Everton v Liverpool
Refa: A Marriner
Refa Wasaidizi: S Ledger, S Bennett
Refa wa Akiba: P Dowd
Newcastle United v West Bromwich Albion
Refa: C Foy
Refa Wasaidizi: H Lennard, R West
Refa wa Akiba: M Halsey
Southampton v Tottenham Hotspur
Refa: L Mason
Refa Wasaidizi: D England, D C Richards
Refa wa Akiba: R East
Chelsea v Manchester United
Refa: M Clattenburg
Refa Wasaidizi: M McDonough, S Long
Refa wa Akiba: M Jones
0 Maoni/comments: