CHELSEA VS MAN-UTD KWA MARA YA TENA!!! FERGUSON AMTAKIA KILA LA KHERI REFA ATAKAYECHEZESHA
Posted in Alex Ferguson, Chelsea, Clattenburg, Lee Mason, Manchester United
Na Wenzetu Soka In Bongo.com

Sir Alex Ferguson amemtakia kila la heri Refa Lee Mason katika Mechi ya Jumatano Oktoba 31 itakayochezwa Uwanja wa Stamford Bridge kati ya Chelsea na Manchester United ikiwa ni Mechi ya Raundi ya 4 ya Mtoano ya CAPITAL ONE CUP ambayo imekuja Siku 3 tu baada ya Timu hizo kupambana kwenye Ligi na Chelsea kuchapwa 3-2 huku Wachezaji wao wawili kutolewa kwa Kadi Nyekundu na wao kubakia kuwasilisha malamiko rasmi kwamba Refa wa Mechi hiyo, Mark Clattenburg [Pichani], alitumia lugha isiyofaa dhidi ya Wachezaji wao.

>>CAPITAL ONE CUP UWANJA: Stamford Bridge JUMATANO SAa 4:45 Usiku

Kwa sasa FA, Chama cha Soka cha England, kimefungua uchunguzi kuhusu tuhuma hizo dhidi ya Refa Clattenburg na wakati huo huo Polisi nao wanafanya uchunguzi wao kuhusu Refa huyo baada ya kupokea malalamiko kutoka Kundi la Wanasheria Weusi kuhusu tuhuma za Ubaguzi za Refa huyo dhidi ya Kiungo wa Chelsea John Mikel Obi na Juan Mata.
Vile vile, Polisi wanachunguza kuumizwa kwa Mlinzi wa Uwanja na Mashabiki wa Chelsea waliporusha vitu Uwanjani kumtupia Javier Hernandez aliekuwa akisherehekea kufunga bao la 3 na la ushindi.
Akiongea na Wanahabari kuhusu Mechi ya CAPITAL ONE CUP na Chelsea, Sir Alex Ferguson aliulizwa kama ana ujumbe wowote kwa Refa Mason, Ferguson alijibu: “Namtakia bahati njema Refa!”
Ni wazi, hasa baada ya matukio ya Mechi ya Jumapili ambayo Chelsea iliwapoteza Branislav Ivanovic na Fernando Torres kwa Kadi Nyekundu, Refa Lee Mason atakuwa akiaangaliwa kwa makini kuhusu uchezeshaji wake.
Akiongelea Timu yake, Sir Alex Ferguson amesema atabadili Wachezaji na huenda Nani, Chicharito, Ryan Giggs, Anderson, Paul Scholes na Danny Welbeck wakacheza pamoja na Chipukizi Scott Wootton, Belgian Marnick Vermijl, Michael Keane na Nick Powell.
Hata Chelsea watalazimika kufanya mabadiliko kwa vile Ivanovic, Torres na John Terry wapo Kifungoni na Frank Lampard ni majeruhi.
SHUKA CHINI KWA RATIBA
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP
RATIBA RAUNDI ya 4:
Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu
Jumanne Oktoba 30
Sunderland v Middlesbrough
Swindon v Aston Villa
Wigan v Bradford
Leeds v Southampton
Reading v Arsenal
Jumatano Oktoba 31
Norwich v Tottenham
Liverpool v Swansea [SAA 5 Usiku]
Chelsea v Manchester United
+++++++++++++++++++++++++
0 Maoni/comments: