Stoke City Yamng'ang'ania M.Owen, Huku Meireles Kuihama Chelsea Kwenda Fenerbahce
Posted in Michael Owen, Raul Meireles
Stoke City yategemea kumsaini Michael Owen
Meneja wa Stoke City Tony Pulis
amebainisha kuwa wapo mbioni kumsaini aliekuwa Straika wa Manchester
United Michael Owen kwa Makataba wa ‘cheza ulipwe.’
Kwa vile Michael Owen ni Mchezaji
‘Huru’, baada ya kuachwa na Manchester United, anaruhusiwa kusaini na
Klabu yeyote licha ya Dirisha la Uhamisho kufungwa juzi Ijumaa Agosti 31
hadi Januari Mwakani na mwanya huo sasa umemfanya Owen awe lulu kwa
Klabu nyingi, hasa Liverpool na Sunderland, ambazo zinasemekana pia
zinamwania.
Klabu ya Uturuki Fenerbahce imetamka
kuwa Mchezaji wa Chelsea ambae pia ni Kiungo wa Kimataifa wa Portugal
Raul Meireles yupo kwao akipimwa afya kabla hajakamilisha Uhamisho.
Fenerbahce wanaruhusiwa kumnunua Kiungo
huyo mwenye umri wa Miaka 29 kwa vile kwao Dirisha la Uhamisho
linafungwa kesho kutwa Jumatano.
Meireles alijiunga na Chelsea Mwaka mmoja uliopita akitokea Liverpool.
0 Maoni/comments: