Nimepoteza Heshima Yangu Kwa Alex Ferguson: Dimitar Berbatov
Posted in Alex Ferguson, Dimitar Berbatov

Aliekuwa Straika wa Manchester Unted
Dimitar Berbatov ambae Ijumaa iliyopita aliuzwa kwa Klabu ya Fulham
ametoa dukuduku lake na kulalamika jinsi alivyotendewa na Meneja wa
Manchester United hadi kulazimika kuhama.
Berbatov, alienunuliwa na Man United
Mwaka 2008 kutoka Tottenham, alikosa namba Msimu uliopita na amedai kuwa
alimfuata Ferguson karibu mara 15 akitaka kujua hatima yake lakini kila
mara alihakikishiwa umuhimu wake.
Berbatov amesema alipoondoka Old Trafford hakuagana na Ferguson kwa vile alipoteza heshima yake kwake.
0 Maoni/comments: