MBWANA SAMATTA, YAYA TOURE, DIDIER DROGBA KUGOMBANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA>> LISTI KAMILI TOKA CAF
Posted in Didier Drogba, Mbwana Samatta, TP Mazembe, Yaya Toure
Shirikisho la Soka Afrika, CAF, limetangaza Majina ya Wachezaji kwenye Listi ya awali ya Wagombea 32 wa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika toka Klabu za Afrika kwa Mwaka 2012 na miongoni mwao ni Staa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, anaechezea TP Mazembe ya Congo DR.
Listi nyingine ni ile ya Wachezaji 34 ambao wanawania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika na hii inao Wachezaji wanaocheza nje ya Afrika akiwemo Yaya Toure wa Manchester City ambae ndie alitwaa Tuzo hii Mwaka jana.
CAF limetangaza kuwa Listi hizo za awali zitapunguzwa hadi Majina 10 kwa wale wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika na 5 toka ile Listi ya kina Mbwana Samatta kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Klabu za Afrika ifikapo mwishoni mwa Oktoba.
Baada ya hapo Majina hayo 15 toka Listi hizo mbili yatawasilishwa kwa Vyama vya Soka vya Nchi Wanachama, Makocha Wakuu wa Timu za Taifa na Makatibu wa Wakuu kuteua Majina matatu kwa kila Listi kutinga Fainali ambapo hapo Desemba 20 Wachezaji Bora watatangazwa na kupewa Tuzo.
Pamoja na Tuzo za Wachezaji Bora pia Kocha Bora na Klabu Bora watazawadiwa Tuzo katika Sherehe maalum hapo Desemba 20 huko Mjini Accra, Ghana.
LISTI za AWALI:
MCHEZAJI BORA wa MWAKA:
- Abdelaziz Barrada - Getafe (Spain) and Morocco
- Adel Taarabt - Queens Park Rangers (England) and Morocco
- Alain Sibiri Traore - Lorient (France) and Burkina Faso
- Alexander Song - Barcelona (Spain) and Cameroon
- Andre 'Dede' Ayew - Marseille (France) and Ghana
- Arouna Kone - Wigan (England) and Ivory Coast
- Aymen Abdennour - Toulouse (France) and Tunisia
- Bakaye Traore - AC Milan (Italy) and Mali
- Cheick Tiote - Newcastle United (England) and Ivory Coast











