WAREMBO 30 WANATEGEMEWA KUINGIA KAMBI YA REDDS' MISS TANZANIA 2012
Posted in Hashim Lundenga, Miss Tanzania, Redds Miss Tanzania 2012
WAREMBO 30 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanatarajiwa kuingia kambini leo kwenye hoteli ya Giraffe kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kushiriki shindano la urembo la Taifa Redd’s Miss Tanzania 2012 litakalofanyika Novemba 3 kwenye ukumbi wa hoteli ya Ubungo Plaza hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency International, Hashim Lundenga alisema kuwa warembo wote walishapewa taarifa za kuripoti kambini leo na mara baada ya kuwasili watapewa taratibu za kambi hiyo.
Lundenga aliwataka washiriki hao kuhakikisha wanawasili asubuhi mapema katika ofisi za Kamati ya Miss Tanzania kama walivyoambiwa ili wapelekwe pamoja katika hoteli hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya kambi yao ya mwezi mzima.
Alisema warembo wakiwa katika kambi ya Redd’s Miss Tanzania watafundishwa mambo mengine muhimu katika maisha yao ambayo yatawafanya wajiandae kuwa wanawake walio na maendeleo na watakaokuwa tayari kuongoza familia zao.











