Hivi ulikuwa unajua kuna msanii wa bongomovie ilikuwa bado kidogo tu
agombee ubunge kwenye jimbo la Ilala, sababu ya kutokugombea ni kwa
kukosa kura chache sana za maoni kutoka kwenye chama chake cha CCM akiwa
mshindi wa pili kwenye kura za moani. Oky, hapa leo nitakupa wasanii wa
bongomovie watatu waliotamka rasmi kwamba mwaka 2015 watagombea ubunge
na mmoja wao itakuwa ni mara yake ya pili kukimbika kiti hiki cha
ubunge.
1.JUMA CHIKOKA “CHOPA MCHOPANGA”
Mchopanga “Juma Chikoka” baada ya kuchuka fomu 2010
Kama ulikuwa hujui kuhusu huyu jamaa ni kwamba, kama mambo
yangemuendea vizuri mwaka 2010. Basi leo hii tungekuwa tunaanza kumuita
na neno muheshimiwa, then jinalake lingefuata. Tena siyo wa jimbo la
dogo, mbunge wa moja kati ya majimbo makubwa hapa Tanzania jimbo la
Ilala. Juma Chikoka akipitia katika chama cha CCM,alifanikiwa kushika
nafasi ya pili kwenye kura za maoni akipishana kura chache na mbunge wa
Ilala maarufu kama “Zungu”. Unaweza kujiuliza juu ya uwezo binafsi
alionao kijana jamaa huyu mkali wa maigizo toka enzi za Kaole kwa
kufanikiwa kufika nafasi ya juu kabisa kwenye kura za maoni kugombea
jimbo gumu na muhimu kama Ilala.
Chopa mchopanga aliwahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni Sharif
shamba na baadaye akiwa India alikuwa mmoja kati ya waanzilishi wa tawi
la CCM India lililozinduliwa na Mhe. Samwel Sitta.Chopa mwenye anaweka
wazi kwamba mwaka 2015 lazima aendeleze harakati kwasababu yeye ni
kiongozi makini na mpenda mabadiliko. Kama ulikuwa hujui kitu kingine
kuhusu Chopa ni kwamba jamaa alimaliza form six pale Tambaza. Baada ya
hapo alipata nafasi ya scholarship kwenda kusoma
India baada ya kufaulu vizuri na kipaji chake cha kuigiza kikimuongezea
credit za kupata hiyo scholarship. Choka amamemaliza degree yake ya
kwanza kwenye chuo cha Bangalore akisomea mambo ya sanaa na mahusiano na
jamii(PR). Kuna mengi ya kuyajua kuhusu Chopa Mchopanga ambayo
haujawahi kusikia wala kuona, endelea kutemebelea website hii utayajua
ambayo hukuwahi kuyajua kuhusu Chopa.Tumeombee uhai,afya njema na hali
hii hii aliyonayo sasa ili 2015 tupate mheshimiwa mwingine kutoka kwenye
sanaa,
2.JACOB STEVEN “JB”

Bonge la bwana, kaka mkuu wa tasnia ya bongomovie na yeye pia ni mmoja
kati ya wasanii ambao wanatarajiwa kugombea ubunge ikifka 2015. Bado
hajaweka wazi atagombea jimbo gani au kupitia chama gani?. Mwaka huu kwa
wasanii wa bongomovie yeye ndiyo alikuwa wa kwanza kutangaza nia yake
ya kugombea ubunge thou vyanzo vyote vya habari bado havijapata kujua ni
jimbo gani ambalo “DJ Ben” ataenda kumwaga sera zake ili mwananchi
wamchague ikiwa ni baada ya kupita kwenye kura za maoni kwanza. Imagine
that, JB yupo ndani ya mjengo..suti kali na kaenea kwenye kiti chote cha
bungeni. Hapo sasa ndiyo zipambe moto harakati za kupambana juu
ya piracy kwenye kazi za wasanii. Kama Chopa,..tunamtakia afya njema JB
na nia yake isibadilike hadi siku ya uchaguzi ikifika ili tumchague awe
mbunge wetu.
3. DEOGRATIOUS SHIJA

Moja kati ya ma-best wakubwa wa marehemu Sajuki, anaitwa Shija. Kwa
upande wake yeye ameweka wazi jinsi atakavyogombani ubunge wake na lengo
kuu la kugombania huo ubunge.Shija yeye anasema kwamba kutokana na
mabadiliko ya katiba yanayoendelea..ni kwamba ana nafasi ya kugombania
ubunge akiwa kama mgombea binafsi. Akiongeza infoz zaidi anasema kwamba
lengo lake kuwa mbunge ni kutetea haki za wanyama baada ya kujifunza
vitu hivyo akiwa Kenya na Uingereza.”Wanyama ni sehemu ya maisha yetu na
viumbe kama sisi, sio kila mbunge aingie bungeni kutetea jimbo lake tu
bali kuna vitu vingi vinaitaji uwakilishi pia”. Duh! Haya sasa, kitu
2015 hiyo mgombea binafsi Shija na sera yake ni kutetea wanyama. Uhai na
afya juu uwe naye ili 2015 afanye kweli.