Next
Previous
Showing posts with label Erasto Msuya. Show all posts

Tuesday, August 13, 2013

0

PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA MISA YA MAZISHI YA ERASTO MSUYA,BILIONEA ALIYEPIGWA RISASI ARUSHA.

Posted in

Familia ya marehemu katika ibada ya kumwaga marehemu Erasto Msuya iliyofanyika  Jumatatu huko  Sakina Arusha.

IMG-20130812-WA0006
Dada wa marehemu Erasto Msuya  katika ibada ya kumwaga marehemu kaka yake Erasto Msuya nyumbani kwake Sakina Arusha.

Thursday, August 8, 2013

0

TAARIFA JUU YA KIFO CHA TAJIRI WA MAWE ARUSHA: ERASTO MSUYA

Posted in ,
Picture
Habari zilizopatikana majira ya saa kumi kasoro robo alasiri jana zinafahamisha kuwa, Mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha na mmiliki wa hoteli amepigwa risasi na watu wasiojulikana bado katika eneo la Mijohoroni upande wa kulia (punde tu baada ya Boma Ng’ombe ukitokea Moshi kuelekea Arusha), mchana wa leo, alipokuwa ameitikia wito alioitiwa wa mazungumzo ya kibiashara ya madini.

 Taarifa zinasema marehemu amepigwa risasi kati ya 6 - 12 katika paji la uso na maeneo mengine ya mwilini.

Mtu mmoja aliyewahi kufika kwenye eneo la tukio baada ya kusikia milio ya risasi anasema alimkuta mtu mmoja wa fanani ya Kimasai ambaye alishuhudia tukio zima na kumsimulia kuwa aliona watu
wanapiga risasi na kisha wakaondoka kwa pikipiki kuelekea porini huku akielekeza mkono kuonesha walikokimbilia. . 

Polisi wanaendelea na uchunguzi baada ya kuuchukua mwili wa marehemu kutoka kwenye eneo la tukio na kuupeleka hospitalini.

Mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Bomang’ombe.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ