HUYU NDIYE NYOTA WA ISIDINGO ALIYEFARIKI DUNIA
Posted in Isidingo, Letty Matabane, South Africa
Lesego Motsepe maarufu kama Letty Matabane ni staa wa tamthilia ya Isidingo ambae uigizaji wake kwenye sehemu kubwa ya tamthilia hiyo ambayo Watanzania wengi wamekua wakiifatilia kupitia ITV.
Taarifa iliyotolewa inasema kaka mtu ndio alimkuta Letty akiwa amefariki nyumbani kwake saa tano asubuhi ambapo kifo chake kilithibitishwa saa kadhaa baadae.
Mwaka 2011 mwishoni Motsepe alitangaza hadharani kuwa amekua akiishi na virusi vya ukimwi kwa karibu miaka 13 na uamuzi huo wa kujitangaza alitaka kuleta mabadiliko na kuwasaidia wale wanaoishi kwenye aina hiyo ya maisha kama yake.
Pamoja na kwamba alijitangaza kuishi na virusi vya ukimwi, chanzo cha kifo chake hakijatangazwa bado.
Ripoti hii imetolewa na Mail & Gurdian.
Source;Keimedia.blogspot.com
0 Maoni/comments: