MAJINA YA WATANZNIA ZAIDI YA 200 AMBAO WANASADIKIWA KUWA WASAMBAZAJI WA BANGI NA MADAWA YA KULEVYA
Majina ya watanzania 255 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya yamejulikana na JAMHURI imeamua kuyachapisha...
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa kwenye orodha hiyo wapo watu maarufu na baadhi wamekuwa wakitoa misaada ,huku wengine wakijifanya ni wazee wa kanisa na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii....
Uchunguzi wetu usio na chembe ya shaka unaonesha kuwa orodha hii ya watu watakaoandikwa hapo chini kwa sasa wapo chini ya uangalizi wa mahakama na polisi..
"Ni kweli kuna watu tumewapeleka mahakamani, huko wamewekwa chini ya uangalizi na wanatakiwa kuripoti kwa muda wanaopangiwa.Tunafanya hivyo baada ya uchunguzi wetu kubaini kwa ni kweli wanahusika na biashara hii haramu."Alisema Nzowa
Nzowa aligoma kuyataja majina hayo, lakini uchunguzi uliofanywa na JAMHURI kutoka ndani ya jeshi la polisi na mahakama umefanikiwa kuyapata majina hayo...
Katika orodha hii, yumo mchungaji aliwekwa chini ya uangalizi , na baada ya kumaliza muda huo, siku tatu baadaye alikamatwa na dawa nchini Brazil.Pia yumo Sheikh anayetoa misaada mbalimbali,lakini baada ya kukamatwa na dawa kilo 211, eneo la Kunduchi Dar es salaam, kwa sasa amekimbilia Afrika kusini....
DAWA ZINAVYOINGIZWA NCHINI:
Hadi sasa kiwango kikubwa cha dawa za kulevya kinaingizwa nchini kwa njia ya meli katika bahari ya Hindi.
Baada ya meli kuwasili Tanzania, wasafirishaji hutumia boti ndogo ziendazo kasi kuchukua dawa hizo.Maeneo yanayotumiwa zaidi kuingiza dawa ni Bagamoyo, Zanzibar, Tanga na Mtwara....
Jijini Dar, boti hizo hutia nanga katika eneo la Bagamoyo ambako pia ndiko kwenye njia kuu ya uingizaji wa bidhaa za magendo zisizolipiwa kodi...
Biashara hiyo haramu huwahusisha baadhi ya polisi ambao mara kadhaa wamekuwa wakiwapa ulinzi wahalifu hao.
Viwanja vya ndege vinavyotumiwa kuingiza madawa ya kulevya ni Julius Nyerere ( DAR ) na Abeid Amani Karume ( ZANZIBAR)
Taarifa toka kitengo cha kuzuia dawa za kulevya zinasema kuwa wasafirisha wanaotumia ndege wamekuwa wakibuni mbinu mbali mbali zikiwemo za kutumia manukato kwa ajili ya kuwapumbaza mbwa wenye mafunzo ya kubaini madawa ya kulevya....
Habari zaidi zinasema kuwa kitengo kimepata vifaa maalumu vya kubaini kama ndani ya mizigo kuna madawa ya kulevya. Vifaa hivyo ni mfano wa sindano ambayo huchomwa kwenye mizigo na kuipitisha kwenye ngozi ya mwili.
Kama kuna dawa, ikigusishwa kwenye ngozi unga hupukutika na kama mzigo hauna dawa za kulevya basi hakuna kitakachotokea....
Tayari vifaa hivyo vimeanza kutumika katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Ifuatayo ni orodha ya wauza unga ambao mahakama imewaweka chini ya uangalizi:
0 Maoni/comments: