Monday, August 12, 2013

0

KUHUSIANA NA KUSACHIWA MADAWA YA KULEVYA: JE NA WASANII WA BONGO MO0VIE KUKUMBWA NA AIBU HIYO??

Posted in , ,
Wema Abraham Sepetu



Hamad Ali




KWELI Waswahili usema kua uyaone, awali nilifikiri mjini ni maghorofa kumbe ni zaidi ya hayo maghorofa, hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongo fleva kupekuliwa Airport, wasanii wa muziki huu kwa sasa si marafiki wa viwanja vya Ndege swali linakuja je wasanii wa filamu nao watapata jeraha hilo?
Kufuatia kashifa ya uvushwaji wa madawa ya kulevya inayolisakama Taifa la Tanzania wasanii wa muziki wa Bongo fleva wamekuwa waathirika wakubwa katika viwanja vya Ndege kwani inapofikiwa wakati wa kupekuliwa wanapekuliwa kweli kweli hadi wengine wanakasirika na kuhisi kama wanadharirishwa kwa kufanyiwa hivyo.
Ambwene YesayaWabongofleva ambao moja kwa moja wameonja adha ya kuhisi wanaweza kuwa na Ngada katika mabegi yao ni pamoja na Ambwene Yesaya AY ambaye alikutana na mkasa huo akiwa uwanja wa ndege na kutumia muda mwingi katika kupekuliwa hadi pale waliporidhika na kuona hana hatia na kuruhusiwa kuendelea na safari yake baada ya kujiridhisha.

Naye Raisi wa Manzese Hamad Ali aka Madee alikutana na kimbembe pale alipotua nchini Afrika ya kusini akiwa sambamba na Mzimbabwe wao pekee ndio waliowekwa kiti moto kwa kupekuliwa zaidi ya saa moja kwa kuvuliwa hadi nguo za nyepesi za ndani na mabegi yao kwa kumwaga nguo zote na baadae kuombwa radhi kwa muda wao na kupekuliwa sana.
Sasa watu wanajiuliza kuwa je hali hiyo kwa upande wa wasanii wa Bongo Movie nao wanaweza kukutwa na adha hiyo ? ya kupekuliwa hadi kutumia zaidi ya muda mrefu hata kudharirishwa kwa kukaribia kuvuliwa kufuli, hakuna anayejua kuhusu hilo kwani wengi wanaamini kuwa inawezekana kwa sababu wanasafiri sana tofauti na waigizaji maswali ni mengi.

Pengine historia nayo inachangia hadi leo kwa wasanii wa filamu hakuna taarifa sahihi kuhusu kashifa ya matumizi ya madawa ya kulevya kwa waigizaji jambo ambalo limekuwa likiripotiwa kila siku kwa wasanii wa Bongo fleva pamoja na watu wao wa karibu kama wapenzi wao na Video queen ambao tayari wamekamatwa na madawa ya kulevya.

Sakata lilianzia pale Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania,


Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, alitarajia kuona utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anayeingia Afrika kusini.

Ukaguzi ambao unafanywa uwanjani (Airport) kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe, lakini hali ilikuwa tofauti kabisa hakuna tena ukaguzi wa kutegemea mashine pekee, Bongo movie pamoja na kuvuma na kuwa na baadhi ya wakina dada kuvuma kumiliki magari mazuri matumizi ya fedha mabaya lakini hamjapoteza imani na watu wa Uhamiaji hongereni kwa hilo.

Ni fedhea kwa msanii kupoteza uaminifu kwani biashara ya muziki inawezekana hapa Bongo hailipi zaidi hivyo msanii akitoka ni rahisi kujiongezea kipato zaidi, pia ni changamoto kwa taasisi za Serikali zinazosimamia wasanii kazi wanazofanya haziwalipi kulingana na wimbi la Maharamia wa kazi zao nao wanahitaji maisha ya kisuperstar wafanyeje? Ndo mana wengi unakuta wanabeba unga..


0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ