Sunday, August 11, 2013

0

HII NDO ATHARI YA KUWEKA PICHA ZA UCHI MTANDAONI

Posted in , ,


Mwezi wa kujistiri kwa wale wenzangu na mie ndiyo huo umeondoka, hapana shaka kuna wengine wanasoma hapa, huku wakiwa ndani ya yale mambo yetu. Siyo ishu, kila mtu ana uhuru wa kufanya kile akipendacho. Nchi yetu inaruhusu kuvaa chochote, ilimradi tu usiende utupu.

Nakumbuka miaka kama mitatu nyuma iliwahi kutokea hoja kuhusu mavazi, wengi walisema Serikali ilikuwa na mpango wa kupiga marufuku vimini na nguo za kubana.

Basi bwana siye tunaopenda mambo hayo roho zilikuwa juu, huku wengine tukitishia hata kuhama nchi ikiwa tutafikia huko kwa kukatazana mavazi.

Lakini kwa bahati nzuri rais wetu, Jakaya Kikwete alilitolea tamko suala hilo  na kusema kuwa kila mtu ana uhuru wa kuvaa kile anachojisikia, ili mradi tu asiende utupu. Hapo alimaliza kila kitu.

Tuachane na mambo ya mavazi, suala la msingi leo ni ‘mapicha’ na tattoo tunazochora mwilini na kuzitupia mtandaoni kila kukicha. Turudi kulekule kwenye uhuru wa kufanya kile unachojisikia, lakini usiku ukienda kulala jiulize mwisho wake nini?

Mimi na wewe hatujui kesho tutakuwa kina nani katika dunia hii, labda uniambie wewe huna ndoto za kufanya jambo litakalokufanya ukumbukwe, hata ukitoweka kwenye uso wa dunia.

Kila mtu, hasa wasichana waona fahari kuweka picha za nusu uchi  katika mitandao ya facebook, twitter na sasa instagram . Ujana, maji ya moto, kwa sasa hizo ‘likes’ na ‘comment’ unazopata zinakuvimbisha kichwa, lakini naamini baadhi yetu, miaka kumi ijayo tutatamani kurudi nyuma ili tuondoe historia mbaya tulioiweka mtandaoni.

Picha hizi zitatumika kukugandamiza kwa chochote unachokusudia kukufanya wakati huo. Ni nani atamchagua kiongozi mwenye picha kama zako unazotupia sasa.Kampuni gani yenye heshima itakayomwajiri mtu mwenye sifa mbaya kwa jamii.



Watu wengi wana uwezo kuona kinachoendelea kwenye mtandao, kumbuka miaka sita au saba kutoka leo siyo mbali, watu watakumbuka, wengine watakuwa na picha zako. Wasiokupenda watazitumia kama silaha ya kukuangamiza.

Kitu kingine ambacho unaweza kuja kukijutia ni hizo tattoo unazochora hivi sasa. Wapo watu hivi sasa wanalazimika kuvaa mashati yenye mikono mirefu, suruali au nguo zenye kuficha maeneo fulani ili waifiche michoro hiyo.

Itafika wakati unashindwa hata namna ya kuwaeleza watoto wako kwa kuwa wengi wanachora kwa kufuata mkumbo au kwa kuona Rihanna, Chris Brown kachora.

Alafu ubaya wengine huchora majina ya wapenzi wao tena sehemu ambazo mtu unaweza kujiuliza alichorwaje,mbaya zaidi ni pale unapochorwa jina la mpenzi wako anaeitwa kwa mfano tuseme Peter alafu unakuja kuolewa labda na George,hivi unafikiri itakuwaje? Sawa wanaume wengine wanaweza wasijali sana lakini je wewe utakuwa unajisikiaje umeolewa na Peter huku umejitattoo George kifuani au kiunoni na haitoki for the rest of ur life kwasababu huwezi kufuta?...
Ni mtazamo tu...

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ