Wednesday, July 31, 2013

0

USAJILI WA SOKA ULAYA: GARETH BALE AFANYWA LULU, KUVUNJA REKODI YA USAJILI

Posted in


>>REAL IMETOA OFA PAUNI MILIONI 85, NI REKODI DUNIANI!
>>MAN UNITED KUVUNJA REKODI YAO KUNUNUA MCHEZAJI BEI JUU!
GARETH_BALE-BARAFUZIPO ripoti kuwa Staa wa Tottenham Gareth Bale leo ameiambia Klabu yake kuwa anataka kujiunga na Real Madrid na huko Old Trafford zipo tetesi Manchester United wanaandaa Ofa yao ya tatu kwa ajili ya kumnunua Cesc Fabregas kutoka Barcelona baada ya mbili za kwanza kukataliwa.
BALE NA REAL
Inadaiwa leo Gareth Bale ameiambia rasmi Tottenham kuwa yeye anataka kuhamia Real Madrid.
Inasemekana leo Bale alitua Mazoezini na pia kuendelea na matibabu yake ya maumivu ya Musuli ambako alimuambia rasmi Meneja wa Tottenham, Andre Villas-Boas, nia yake ya kuhamia Real.
Zipo taarifa kuwa Real Madrid wametoa Ofa ya Pauni Milioni 85 kumnunua Bale, ambayo ni Rekodi ya Dunia, lakini hadi sasa Tottenham hawajasema lolote kuhusu hilo licha ya kukana huko nyuma kwamba Mchezaji huyo hauzwi.
Hivi majuzi, Villas-Boas alisema anatarajia Bale atakuwa fiti kucheza Mechi yao ya Kirafiki hapo Jumamosi na Monaco ya France.
Wakati hayo yakinong’onwa, Mchezaji mmoja wa zamani wa Spurs, Jamie Redknapp, alitafakari: “Real Madrid ni Klabu kubwa Duniani, hawezi Bale kuikataa! Na naamini Tottenham ni Klabu inayouza Wachezaji wake wakubwa, historia yao inasema hivyo! Angalia nyuma Michael Carrick, Modric na Berbatov, waliuzwa! Wanauza kwa Bei muafaka kwao!”CESC_FABREGAS

MAN UNITED WATAFAKARI OFA MPYA FABREGAS!
Inaelekea Manchester United bado hawajakata tamaa kumnasa Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas na zipo ripoti kuwa sasa wanatayarisha Ofa ya tatu baada ya mbili kukataliwa na hii ya tatu inaelekea itavunja Rekodi yao Bei ya juu ya kumnunua Mchezaji ambayo ilikuwa Pauni Milioni 30.75.
Tayari Ofa mbili za Man United, ile ya Pauni Milioni 25 na nyingine Milioni 30, zimekataliwa na Barcelona kwa ajili ya kumnunua Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal.


MAN UTD: BEI JUU KUNUNUA MCHEZAJI:
-Dimitar Berbatov (Tottenham) £30.75m
-Rio Ferdinand (Leeds) £30m
-Juan Sebastian Veron (Lazio) £28.1m
-Wayne Rooney (Everton) £27m
-Robin van Persie (Arsenal) £24m

Licha ya kukataliwa mara mbili, ripoti zinadai kuwa Man United bado wana imani ya kumnasa Fabregas.
Hata hivyo, ripoti hizo pia zinadai kuwa ikiwa Man United watakwama kumchukua Fabregas watawageukia Kiungo wa Everton Marouane Fellaini au yule wa Real Madrid, Luka Modric.
Hadi sasa, kwenye Kipindi hiki cha Uhamisho, Man United wamesaini Mchezaji mmoja tu ambae ni Beki Chipukizi wa Uruguay, Guillermo Varela ingawa Meneja David Moyes bado ana imani kubwa ya kupata wapya.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ